Wakuu nakuja kwenu kuomba ufafanuzi wa maswali yangu haya machache kuhusu nchi ya Israeli.
Mimi mpaka Leo nimeshindwa kupata majibu ya haya maswali yangu.
•Kuna baadhi wanasema nchi wanayoishi Israeli sio ya kwao bali waliwapora wapalestina,je Kama hapo wanapoishi waisraeli sio pao,je kwao(ardhi) yao ni ipi?
•Je,ile nchi ya ahadi aliyoahidiwa ibrahimu na Mungu ni ipi na iko wapi na ni nani anayeimiliki kwa sasa?
Na anaye imiliki kwa sasa ni haki yake?
•Kuna nadharia inayosema kuwa waisraeli walikuwa ni WEUSI.Je,hao waisraeli weusi kwa sasa wako wapi?
Na hapo wanapoishi ndio hiyo nchi ya AHADI waliyo ahidiwa na Mungu kupitia kwa Ibrahimu?
•Upi ushahidi kuwa waisraeli walikuwa ni weusi na nini kimetokea kwa sasa wasiwe weusi wakawa weupe?
Asanteni
Majibu ya maswali yako ni kama ifuatavyo
1.Swali la kwanza (
"Kuna baadhi wanasema nchi wanayoishi Israeli sio ya kwao bali waliwapora wapalestina,je Kama hapo wanapoishi waisraeli sio pao,je kwao(ardhi) yao ni ipi?')
Kabla sijalijibu tunatakiwa tujue historia ya hili taifa inaanzia wapi,kwenye biblia hili taifa lilianzia kwa baba yao wa kwanza alikuwa anaitwa Abraham.Huyu Abraham alikuwa ni mwenyeji wa nchi ya "URU WA WAKALDAYO" kwa mujibu wa ramani za ki biblia URU ni mji uliokuwa unakaliwa na wakaldayo na kwa dunia ya leo hilo eneo la uru lipo kwenye nchi ya IRAQ.
Mungu alimtokea Abraham (
Mwanzo 12:1-3 "
BWANA akamwambia Abrahamu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa" )
Abraham akatii kama Mungu alivyomwambia akatoka Uru akaenda kanaani (
Mwanzo 12:5 "
Abrahamu akamchukua Sarai mkewe, na Lutu mwana wa nduguye, na vitu vyao vyote walivyokuwa wamejipatia na hao watu waliowapata huko Harani, wakatoka ili kwenda nchi ya Kanaani; nao wakaingia katika nchi ya Kanaani " wakiwa huko kanaani Mungu alimwambia hii nchi atampa Abraham yeye na uzao wake woote
Mwanzo 12:7 ,ndio huko kanaani Abraham aliishi na mwanaye wa pekee
ISAKA na baadaye Mjukuu wake
YAKOBO ambaye baadaye alibadirishwa jina akaitwa
ISRAEL.Huyu Israel (Yakobo) na watoto wake 12 walikuja wakakimbilia Misri kujiokoa na njaa iliyokuwa imeikumba nchi ya kanaani wakakaa huko miaka 430 wakawa watumwa huko baadaye Mungu kupitia Musa akawarudisha tena kwenye Nchi aliyomwahidi baba yao Abraham ili kulitunza agano lake akawarudisha kanaani tena.
Kufafanua vizuri zaidi kwenye hiyo ardhi ya kanaani kulikuwa na mataifa mengi sana yanaishi humu ikiwamo na hao wakanani pia (
Mwanzo 15:18),na wakati mwingine idadi ya haya mataifa ilikuwa inabadirika mara kwa mara kwenye biblia.Nirudi kwenye swali lako Jibu lipo hivi
Waisraeli (sio hawa wa sasahivi) wanasema ile pale ni ardhi yao sababu Mungu aliwapa kupitia agano lake na baba yao Abraham,na yale mataifa wazawa wa kanaani kwa kuwa hawamwamini huyo Mungu wa israel nao pia wanaona ile bado ni ardhi yao na ndiomaana tangia Joshua ameingia kanaani hadi enzi za nabii Malaki kumekuwa na vita baina ya wana wa israeli na wana wa wakanaani ikumbukwe sasa ndani ya wana wa wakanaani kuna mchanganyiko wa mataifa(vizazi,falme) mbali mbali,sasa kwakuwa tunamwamini Mungu basi tunaamini ile pale ni ardhi ya wana wa Israeli sababu ndiye aliye wapa.
Weka akilini sijasema hawa wapalestina ndio miongoni mwa vizazi vizaliwa vya wakanani,na wala sio wapalestina ndio wafilisti hakuna mahala kwenye biblia pamesema hivyo.
2.Swali la pili (
•Je,ile nchi ya ahadi aliyoahidiwa ibrahimu na Mungu ni ipi na iko wapi na ni nani anayeimiliki kwa sasa?Na anaye imiliki kwa sasa ni haki yake?)
Hili swali kwa maelezo niliyoyaeleza hapo juu yanatosha kulijibu,kwa haraka nifafanue mipaka ya nchi aliyoahidiwa ibrahimu.Kwenye biblia kuna mipaka ya aina mbili ya taifa la israeli
>Mpaka wa kwanza unaanzia kwenye
mto Nile pale Misri mpaka mto Euphrates(mto flati) Iraq
Mwanzo 15:18 (
Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati")
>Mpaka wa pili unaanzia
Dan Mpaka Baarsheva ,Waamuzi 20:1,1Samweli 3:20,2Samweli 3:10,2Samweli 17:11,1Nyakati 21:2,
Sasa hii ramani ya ardhi ya isareli sasa hivi inataka kufanana kidogo na hii ya (Dan mpaka Baarsheva) na ndiyo wana wa israel walikuwa wanaitumia baada ya kuingia kanaani na Joshua na kuendelea na kabla ufalme wa israel haujagawanyika baada ya kifo cha mfalme Suleiman.
3.Swali la tatu (
Kuna nadharia inayosema kuwa waisraeli walikuwa ni WEUSI.Je,hao waisraeli weusi kwa sasa wako wapi?Na hapo wanapoishi ndio hiyo nchi ya AHADI waliyo ahidiwa na Mungu kupitia kwa Ibrahimu?"
Hii kitu nimewahi kuielezea kwa undani sana kwenye thread niliandika hapa JF inaitwa uhalisia wa Taifa la israel link hii hapa chini kaisome
Uhalisia wa taifa la Israeli
Ila kwa haraka nitajibu kama ifuatavyo,Wana wa israel walikuwa ni watu wa rangi,hapa namaanisha walikuwa sio watu wa rangi moja (White/wazungu) bali walikuwa na rangi mchanganyiko,ni mtu mweusi tu ndio ana ngozi ya rangi tofauti tofauti,mfano kuna watu weusi ila ngozi yao ni nyeupe pee,kuna watu weusi ila wana ngozi Nyeusi tii,nyekundu,brown nk..
Kwenye biblia kuna baadhi ya manabii wamejieleza rangi zao kama nyeusi
Ayubu 30:30, Mfalme Suleiman kasema pia ni mweusi kwenye
Wimbo ulio bora 1:5 ,wimbo ulio bora 1:6, Na baadhi ya wengine wamesema kuhusu rangi ya ngozi zao hapa Maombolezo 4:8,maombolezo 5:10 .
4.Swali la Mwisho (•Upi ushahidi kuwa waisraeli walikuwa ni weusi na nini kimetokea kwa sasa wasiwe weusi wakawa weupe?)
Hili swali linajibiwa na hiyo link nimeshare hapo juu na pia na jibu la swali la tatu.Kiharaka haraka wale wazungu (akina netanyahu) unaowaona leo pale israel wanasema wao ni wayahudi (wana wa israel) wale sio wale kwao ni ulaya wale ni fake tu wamewekwa pale na shetani kwa malengo yake ambayo yatakuja kutimia siku za mbeleni kabla hajaja Yesu kwa mara ya pili,wayahudi halisi bado hawajarudi pale israel kama maandiko yanavyosema
zitto junior