fidel castro wapili
JF-Expert Member
- Mar 18, 2017
- 3,497
- 2,911
Wale ni wavamizi. Wamevamia nakuunda lile TAIFA 1946 wakati nabii IBRAHIM aliisha kufa karne kadhaa zilizopita.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Abraham hakupewa Israel,hajawahi kuwa muisrael,na amekufa akiwa hajawahi kusikia kitu kinaitwa Israel,ama uyahudi.Rejea kuu ya historia ya Israel ni Biblia hususani kitabu cha Mwanzo. Ibrahim ndiye Babu wa Israel. Mungu alimfanya kuwa Baba wa Taifa kubwa Israel (Mwa 22). Ibrahim alipewa nchi ya Kanaani (Israeli ya Leo - Mwanzo 13). Baadaye Mungu aliwatoa akawapeleka Misri kupitia Yusufu (Mwa 39-50). Alikuwa amemweleza Ibrahim jambo hili hapo awali na kuwaambia watakaa huko miaka 400 kisha atawarudisha tena Kanaani (Mwanzo 15). Hivyo aliwapa nchi, akawatoa toka nchi hiyo kwa muda (miaka 400), kisha akawarudisha tena nchini mwao kupitia Mussa (Kut 3). Akawasafirisha kurudi nchini mwao kwa miaka 40 kupitia Bahari ya Shamu (Kut 13-14) jangwani (vitabu vya Kutoka, Hesabu, Walawi, Kumbukumbu la Torati na Joshua) wakiongozwa na Musa na baadaye Joshua. Musa wito wake kuwatoa Misri na Yoshua kuwaongoza kuvuka Yordani na kuwarithisha nchi yao (Joshua 1 - 24). Hii ndiyo iliyoitwa nchi ya Ahadi waliyopewa Israeli. Yoshua aliambiwa awatoe wakazi wa humo waliovamia wakati Israeli yupo utumwani Misri. Hao walikuwa Wahiti, Waperizi, Wayebusi, Wakanaani, Waamori, Wakenizi, na Wahivi. Aliambiwa awapigie (awafute na kuwatowesha kabisa). Yoshua aliwaacha baadhi yao. Hao waliisumbua Israel miaka mingi sana.
Israeli hawakupora nchi ile. Walipewa na Mungu. Alipewa Ibrahimu baba ya Israeli wote. Israeli ni Waaramu toka mwanzo yaani Wasemiti. Sio weusi kwa maana ya Uafrika ila sio Wazungu ( caucasian). Tunajua kuwa wapo "Black Jews" ama Wayahudi weusi; yaani "Falasha Jews". Hawa wapo Ethiopia na wengine walihamishiwa Israeli kupitia "Operesheni Musa" ya miaka ya sabini.
Nchi ya ahadi ni ile Israeli ya leo. Kitabu cha Yoshua kinafafanua sana mipaka hiyo kwa kina
1.Je baada ya maangamizi ya Jerusalem,tunaambiwa wayahudi walitawanyika kwenda nchi mbalimbali,Je walikwenda nchi gani/bara lipi.Majibu ya maswali yako ni kama ifuatavyo
1.Swali la kwanza ("Kuna baadhi wanasema nchi wanayoishi Israeli sio ya kwao bali waliwapora wapalestina,je Kama hapo wanapoishi waisraeli sio pao,je kwao(ardhi) yao ni ipi?')
Kabla sijalijibu tunatakiwa tujue historia ya hili taifa inaanzia wapi,kwenye biblia hili taifa lilianzia kwa baba yao wa kwanza alikuwa anaitwa Abraham.Huyu Abraham alikuwa ni mwenyeji wa nchi ya "URU WA WAKALDAYO" kwa mujibu wa ramani za ki biblia URU ni mji uliokuwa unakaliwa na wakaldayo na kwa dunia ya leo hilo eneo la uru lipo kwenye nchi ya IRAQ.
Mungu alimtokea Abraham (Mwanzo 12:1-3 "BWANA akamwambia Abrahamu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa" )
Abraham akatii kama Mungu alivyomwambia akatoka Uru akaenda kanaani (Mwanzo 12:5 "Abrahamu akamchukua Sarai mkewe, na Lutu mwana wa nduguye, na vitu vyao vyote walivyokuwa wamejipatia na hao watu waliowapata huko Harani, wakatoka ili kwenda nchi ya Kanaani; nao wakaingia katika nchi ya Kanaani " wakiwa huko kanaani Mungu alimwambia hii nchi atampa Abraham yeye na uzao wake woote Mwanzo 12:7 ,ndio huko kanaani Abraham aliishi na mwanaye wa pekee ISAKA na baadaye Mjukuu wake YAKOBO ambaye baadaye alibadirishwa jina akaitwa ISRAEL.Huyu Israel (Yakobo) na watoto wake 12 walikuja wakakimbilia Misri kujiokoa na njaa iliyokuwa imeikumba nchi ya kanaani wakakaa huko miaka 430 wakawa watumwa huko baadaye Mungu kupitia Musa akawarudisha tena kwenye Nchi aliyomwahidi baba yao Abraham ili kulitunza agano lake akawarudisha kanaani tena.
Kufafanua vizuri zaidi kwenye hiyo ardhi ya kanaani kulikuwa na mataifa mengi sana yanaishi humu ikiwamo na hao wakanani pia (Mwanzo 15:18),na wakati mwingine idadi ya haya mataifa ilikuwa inabadirika mara kwa mara kwenye biblia.Nirudi kwenye swali lako Jibu lipo hivi
Waisraeli (sio hawa wa sasahivi) wanasema ile pale ni ardhi yao sababu Mungu aliwapa kupitia agano lake na baba yao Abraham,na yale mataifa wazawa wa kanaani kwa kuwa hawamwamini huyo Mungu wa israel nao pia wanaona ile bado ni ardhi yao na ndiomaana tangia Joshua ameingia kanaani hadi enzi za nabii Malaki kumekuwa na vita baina ya wana wa israeli na wana wa wakanaani ikumbukwe sasa ndani ya wana wa wakanaani kuna mchanganyiko wa mataifa(vizazi,falme) mbali mbali,sasa kwakuwa tunamwamini Mungu basi tunaamini ile pale ni ardhi ya wana wa Israeli sababu ndiye aliye wapa.
Weka akilini sijasema hawa wapalestina ndio miongoni mwa vizazi vizaliwa vya wakanani,na wala sio wapalestina ndio wafilisti hakuna mahala kwenye biblia pamesema hivyo.
2.Swali la pili (•Je,ile nchi ya ahadi aliyoahidiwa ibrahimu na Mungu ni ipi na iko wapi na ni nani anayeimiliki kwa sasa?Na anaye imiliki kwa sasa ni haki yake?)
Hili swali kwa maelezo niliyoyaeleza hapo juu yanatosha kulijibu,kwa haraka nifafanue mipaka ya nchi aliyoahidiwa ibrahimu.Kwenye biblia kuna mipaka ya aina mbili ya taifa la israeli
>Mpaka wa kwanza unaanzia kwenye mto Nile pale Misri mpaka mto Euphrates(mto flati) Iraq Mwanzo 15:18 (Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati")
>Mpaka wa pili unaanzia Dan Mpaka Baarsheva ,Waamuzi 20:1,1Samweli 3:20,2Samweli 3:10,2Samweli 17:11,1Nyakati 21:2,
Sasa hii ramani ya ardhi ya isareli sasa hivi inataka kufanana kidogo na hii ya (Dan mpaka Baarsheva) na ndiyo wana wa israel walikuwa wanaitumia baada ya kuingia kanaani na Joshua na kuendelea na kabla ufalme wa israel haujagawanyika baada ya kifo cha mfalme Suleiman.
3.Swali la tatu (Kuna nadharia inayosema kuwa waisraeli walikuwa ni WEUSI.Je,hao waisraeli weusi kwa sasa wako wapi?Na hapo wanapoishi ndio hiyo nchi ya AHADI waliyo ahidiwa na Mungu kupitia kwa Ibrahimu?"
Hii kitu nimewahi kuielezea kwa undani sana kwenye thread niliandika hapa JF inaitwa uhalisia wa Taifa la israel link hii hapa chini kaisome
Uhalisia wa taifa la Israeli
Ila kwa haraka nitajibu kama ifuatavyo,Wana wa israel walikuwa ni watu wa rangi,hapa namaanisha walikuwa sio watu wa rangi moja (White/wazungu) bali walikuwa na rangi mchanganyiko,ni mtu mweusi tu ndio ana ngozi ya rangi tofauti tofauti,mfano kuna watu weusi ila ngozi yao ni nyeupe pee,kuna watu weusi ila wana ngozi Nyeusi tii,nyekundu,brown nk..
Kwenye biblia kuna baadhi ya manabii wamejieleza rangi zao kama nyeusi Ayubu 30:30, Mfalme Suleiman kasema pia ni mweusi kwenye Wimbo ulio bora 1:5 ,wimbo ulio bora 1:6, Na baadhi ya wengine wamesema kuhusu rangi ya ngozi zao hapa Maombolezo 4:8,maombolezo 5:10 .
4.Swali la Mwisho (•Upi ushahidi kuwa waisraeli walikuwa ni weusi na nini kimetokea kwa sasa wasiwe weusi wakawa weupe?)
Hili swali linajibiwa na hiyo link nimeshare hapo juu na pia na jibu la swali la tatu.Kiharaka haraka wale wazungu (akina netanyahu) unaowaona leo pale israel wanasema wao ni wayahudi (wana wa israel) wale sio wale kwao ni ulaya wale ni fake tu wamewekwa pale na shetani kwa malengo yake ambayo yatakuja kutimia siku za mbeleni kabla hajaja Yesu kwa mara ya pili,wayahudi halisi bado hawajarudi pale israel kama maandiko yanavyosema
zitto junior
Kama hakupewa Israel alipewa nini?,Na je jina hili Israel lilianzia wapi,historia yake ni ipi?Abraham hakupewa Israel,hajawahi kuwa muisrael,na amekufa akiwa hajawahi kusikia kitu kinaitwa Israel,ama uyahudi.
Sasa angeweza vipi kupewa kitu ambacho hakikuwepo?
THINK
aonamku umeamua kukazia swali ila kama umejibu kipande cha wao ni weusi ama weupe japo hujawa waziAlikuwa anaitwa Nasser huyo rais wa Misri.
Ikumbukwe Israel walikuwa wametengewa eneo la kuishi Uganda. Ila dakika za jioni Churchill na soros wakafanikisha kupata hicho kipande cha ardhi walipo saivi chini ya Balfour agreement.
Swali; iweje weupe wa rangi watake kujichanganya katikati ya bara la Africa kwa weusi? Wangeweza vipi kujichanganya na kushirikiana na sisi na walikuwa washatutengenezea ubaguzi mkali?
Je' hawakujua ngozi zao ni dhaifu hazina melanin ila bado wakataka kuja kuishi ukanda wa joto karibu na ikweta hapo Uganda?
Ni kitu gani kiliwabadilisha mawazo dakika za jioni na kukacha kuja Africa na kubaki hapo mashariki ya kati?
Mbona ni kazi rahisi sana kupata jibu?,just anza kusoma habari ya Abraham,kwa makini,Kama hakupewa Israel alipewa nini?,Na je jina hili Israel lilianzia wapi,historia yake ni ipi?
Mbona ni kazi rahisi sana kupata jibu?,just anza kusoma habari ya Abraham,kwa makini,
Abraham aliambiwa nchi hii,nitawapa uzao wako,na watakuwa wengi kama mchanga.
Hiyo ni kwa ufupi,hakuambiwa nchi hii nitaupa uzao wako Israel,habari ya caanan kupewa Israel ilianza na Jacobo hata babake isaaka haijui.
Uzao wa Abraham ni mpana sana,na umeenea mpaka MTO frati,hadi Nile Kule.
Uzao wa Abraham ni wana wa wake wote watatu wa abraham
Nikurekebishe hapa,kulikuwa na makabila 12,lakini ni mawili tu ndo yalijulikana kama wayahudi,1.Je baada ya maangamizi ya Jerusalem,tunaambiwa wayahudi walitawanyika kwenda nchi mbalimbali,Je walikwenda nchi gani/bara lipi.
2.Wayahudi hawa wa sasa,uko walipotoka ulaya walikuwa wanadumisha tamaduni,dini,lugha ya kiebrani/kiyahudi?,If not,je Lugha hii na dini hii wameitoa wapi,ni nani aliwafundisha?.
3.Biblia inasema kulikuwa na makabila 12 ya wana wa Israel na wote walijulikana kama wayahudi,Je walikuwa na Rangi moja wote?.
4.Je ni kweli Hittler aliua wayahudi?,kama hakuua wayahudi waliua watu gani na kwa nini?.Na kama ni wayahudi je walikuwa na Rangi gani?.
Hahaha.. Sidhani Kama nimejibu kuhusu rangi! Ila nimependa your instincts! Mapokeo ni mabaya sana!n
aonamku umeamua kukazia swali ila kama umejibu kipande cha wao ni weusi ama weupe japo hujawa wazi
Bila shaka wewe utakuwa professor uko detailed sana huachi kitu nyuma!! Labda tukiachana na mtazamo wa kidini mkuu je ni haki wayahudi wanavyowatreat wapalestina na kama ni sawa kosa lao ni nni hao palestina kwa Mungu hadi aruhusu wachinjwe hivyoRejea kuu ya historia ya Israel ni Biblia hususani kitabu cha Mwanzo. Ibrahim ndiye Babu wa Israel. Mungu alimfanya kuwa Baba wa Taifa kubwa Israel (Mwa 22). Ibrahim alipewa nchi ya Kanaani (Israeli ya Leo - Mwanzo 13). Baadaye Mungu aliwatoa akawapeleka Misri kupitia Yusufu (Mwa 39-50). Alikuwa amemweleza Ibrahim jambo hili hapo awali na kuwaambia watakaa huko miaka 400 kisha atawarudisha tena Kanaani (Mwanzo 15). Hivyo aliwapa nchi, akawatoa toka nchi hiyo kwa muda (miaka 400), kisha akawarudisha tena nchini mwao kupitia Mussa (Kut 3). Akawasafirisha kurudi nchini mwao kwa miaka 40 kupitia Bahari ya Shamu (Kut 13-14) jangwani (vitabu vya Kutoka, Hesabu, Walawi, Kumbukumbu la Torati na Joshua) wakiongozwa na Musa na baadaye Joshua. Musa wito wake kuwatoa Misri na Yoshua kuwaongoza kuvuka Yordani na kuwarithisha nchi yao (Joshua 1 - 24). Hii ndiyo iliyoitwa nchi ya Ahadi waliyopewa Israeli. Yoshua aliambiwa awatoe wakazi wa humo waliovamia wakati Israeli yupo utumwani Misri. Hao walikuwa Wahiti, Waperizi, Wayebusi, Wakanaani, Waamori, Wakenizi, na Wahivi. Aliambiwa awapigie (awafute na kuwatowesha kabisa). Yoshua aliwaacha baadhi yao. Hao waliisumbua Israel miaka mingi sana.
Israeli hawakupora nchi ile. Walipewa na Mungu. Alipewa Ibrahimu baba ya Israeli wote. Israeli ni Waaramu toka mwanzo yaani Wasemiti. Sio weusi kwa maana ya Uafrika ila sio Wazungu ( caucasian). Tunajua kuwa wapo "Black Jews" ama Wayahudi weusi; yaani "Falasha Jews". Hawa wapo Ethiopia na wengine walihamishiwa Israeli kupitia "Operesheni Musa" ya miaka ya sabini.
Nchi ya ahadi ni ile Israeli ya leo. Kitabu cha Yoshua kinafafanua sana mipaka hiyo kwa kina
1.Je baada ya maangamizi ya Jerusalem,tunaambiwa wayahudi walitawanyika kwenda nchi mbalimbali,Je walikwenda nchi gani/bara lipi.
2.Wayahudi hawa wa sasa,uko walipotoka ulaya walikuwa wanadumisha tamaduni,dini,lugha ya kiebrani/kiyahudi?,If not,je Lugha hii na dini hii wameitoa wapi,ni nani aliwafundisha?.
3.Biblia inasema kulikuwa na makabila 12 ya wana wa Israel na wote walijulikana kama wayahudi,Je walikuwa na Rangi moja wote?.
4.Je ni kweli Hittler aliua wayahudi?,kama hakuua wayahudi waliua watu gani na kwa nini?.Na kama ni wayahudi je walikuwa na Rangi gani?.
Unaangalia Israel ya 2018. Umesahau Israel kama jina lilianza Mwa 33. Jina hili alipewa Yakobo mjukuu wa Ibrahimu kwa Isaka mwanawe wa pekee kwa Sarah. Unahitaji kusoma Historia ya Israel ndipo tutaelewana.Abraham hakupewa Israel,hajawahi kuwa muisrael,na amekufa akiwa hajawahi kusikia kitu kinaitwa Israel,ama uyahudi.
Sasa angeweza vipi kupewa kitu ambacho hakikuwepo?
THINK
Columbus ama Amerigo Vespucci alipovumbua America alikuta watu ama hawakuwepo?ibrahimu alipokwenda kwa mara ya kwanza kwenye hiyo nchi ya ahadi alikuta watu au akukuta watu?
Nashukuru Zitto Junior kwa heshima ulionipa. Nimeingia tu nyumbani nikitulia nitajaribu kujibu maswali yako mazuri.Bila shaka wewe utakuwa professor uko detailed sana huachi kitu nyuma!! Labda tukiachana na mtazamo wa kidini mkuu je ni haki wayahudi wanavyowatreat wapalestina na kama ni sawa kosa lao ni nni hao palestina kwa Mungu hadi aruhusu wachinjwe hivyo
Na tukirudi kwa Joshua je ni kwanni Mungu aliamuru aue wacanaan wote?? Kosa lao ni lipi mkuu kiasi hadi vitoto vichanga vilichinjwa??
Kingine kibiblia nchi ya ahadi inaanzia misri hadi iraq je kwanni wayahudi hawaendi kuidai misri na iraq ila wamegandia israel pekee??
Ubarikiwe mkuu
Mimi naongea from historically standing point,Abraham hafahamu chochote kuhusu Israel,bado tu sijaconfirm kama Isaac nae alikuwa bado hai kipindi Jacob anaitwa Israel au nae hana idea Israel ni nini.Unaangalia Israel ya 2018. Umesahau Israel kama jina lilianza Mwa 33. Jina hili alipewa Yakobo mjukuu wa Ibrahimu kwa Isaka mwanawe wa pekee kwa Sarah. Unahitaji kusoma Historia ya Israel ndipo tutaelewana.
Ukitaka kuelimika uwe *objective" zaidi ya kuwa "subjective." Sasa tukuambie ile haikuwa familia tu. Ibrahimu mi baba wa Taifa la Israel. Yakobo ambaye ndie Israeli mwenyewe ni mjukuu wa Ibrahimu. Mungu alimpomtokea Musa (Kutoka 3) alijitambulisha kwa majina hayo "Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo." Hiyo ndiyo "Link" tunayotumia humu. MUNGU ndiye aliyesema Ibrahimu atakuwa taifa kubwa "Mwa 22". Sio sisi. Historia ya Israel nje na ndani ya Biblia imedhihirisha hilo. Msikilize sana Netanyahu anapozungumza. Hakosi kuwataja mababa wa Israel hao watatu. Humtaja hata Daudi. Hujivunia link hiyo ya kihistoria.Mimi naongea from historically standing point,Abraham hafahamu chochote kuhusu Israel,bado tu sijaconfirm kama Isaac nae alikuwa bado hai kipindi Jacob anaitwa Israel au nae hana idea Israel ni nini.
Uhakika nilionao,hadi Isaac anakufa,family yake ilikuwa ni family tu,na wala so watawala wa eneo hilo