Ipi ilikuwa sababu ya kuachana na uliempenda sana?

Ipi ilikuwa sababu ya kuachana na uliempenda sana?

Mimi nilishaachwa, kuacha, na kuachanishwa. Kwenye kuachwa mara ya kwanza ilikuwa ni sababu ya umaskini. Kuna wakati baada ya kumaliza chuo nilivurugwa na maisha nikawa sina ajira, biashara wala chanzo chochote cha pesa. Kimsingi nilikuwa ninanuka umaskini. Nakumbuka kuna wiki fulani nilikuwa nakula kwenye makambi ya wasabato kwa sababu hali ilikuwa tete. Mungu awabariki sana hawa watu wa Mungu.

Kwenye kuacha sababu kuu ni vizinga na kudanganywa kuwa ni bikra. Nakumbuka alitegea siku anaingia hedhi anipe mchezo ili amalize kesi yake ila alikosea kidogo sana mwanzoni kwa kuropoka kuwa hiyo siku anaingia hedhi. Nikajiuliza kwanini huyu manzi leo ndo anipe gemu wakati kila mara amekuwa mgumu? Sikufanya chochote maana pia hisia zilikata kabisa.

Kuachanishwa ni pale nilipopata mtu ninayempenda nikata nimuoe ila familia yake nzima hadi baadhi ya majirani wakakaa naye chini na kumwambia yule kijana hatuifahamu vizuri familia yake hivyo achana naye. Hii ilichangiwa na kuwa manzi kwao matajiri mno.
He Kumbe wewe ni Me!
 
1.Tulifikia hatua ya posa kabisa ila alipoonyesha dharau kwa washenga, nikatoka nduki. (Maswala ya mila na tamaduni zao ilikuwa sababu )

2. Alianza kutongozana na Baba angu mdogo. Nikaona isiwe kesi nikazima data.

3. Dharau tu, miadi ya saa 7 yeye anafika saa9 pasina kutoa udhuru.

(Nikajipatia mhehe wangu mshamba mshamba nikaweka ndani. Nakula raha za elimu akhera)
Upendo ni kitu cha thamani ukikutana na watu sahih bt hayana maana ukikutana na matapeli.

bahati mbaya sana ni ngum kumjua tapeli kwa kumuona.
 
Mimi nilishaachwa, kuacha, na kuachanishwa. Kwenye kuachwa mara ya kwanza ilikuwa ni sababu ya umaskini. Kuna wakati baada ya kumaliza chuo nilivurugwa na maisha nikawa sina ajira, biashara wala chanzo chochote cha pesa. Kimsingi nilikuwa ninanuka umaskini. Nakumbuka kuna wiki fulani nilikuwa nakula kwenye makambi ya wasabato kwa sababu hali ilikuwa tete. Mungu awabariki sana hawa watu wa Mungu.
Pole mkuu, umaskini haufai kabisa.
 
Back
Top Bottom