kwa uelewa wangu mimi, inategemea na shughuli inayotaka kufanyika kazi hiyo pikipiki, na inategemea na maeneo unayotaka kufanyia kazi. interms of power zote zinanguvu sawa coz cylinder capacity (cc) zake ni sawa.
facts
ABIRIA.
. kwa upande wa kubeba abiria maeneo ya tambalale na changamoto kidogo ni vema ukatumia boxer coz suspension system yake + plus seat designing havimuumizi abiria wala kumpa uchovu wa mapema....
ila kwa sanlg (inategemea na model) huwa haipo comfortable sana kwa abiria coz 1... seat designing na rest foot ipo karibu sana hivo abiria anakaa kama kajikunja.. 2.... suspension system ya sunlg huwa ni ngumu hivyo kama mtapita maeneo yenye vishimo ni lazima abiria atateseka. Ndio maana wadada wengi mjini hawapendi kupanda sanlg, fecon, n.k wanaita malori.
MIZIGO.
. Kwa upande wa ubebaji mzigo boxer inauwezo wa kubeba hata kilo 200 na mzigo ukakaa vizuri kwenye seat na pikipiki isilalamike. pia ina faida ya kuwa na vichuma vingi vya katika seat kuruhusu mipira au kamba kufunga mzigo ukae vizuri kwenye carrier au seat. lakini inachangamoto jinsi ilivyoundwa ni nyepesi kwa suspension za mbele kuinuka kama utabeba mzigo mzito na kupita nayo kwenye muiniko au hata mashimo ya barabarani.
sunlg ni nzuri kwa kubeba mizigo mizito kutokata na umbile lake ( imetitia) na mfumo wa gear umerahisishwa ili kihimili mizigo mizito mf. gear no 1 inanguvu kwa kuwa ina mzunguko mkubwa chukulia mfano gear no 1 ya scania na ya landcruiser utaona kuna utofauti wa rpm ya engine na speed ya final drive. pia muundo ya pkpk jinsi ulivotengenezwa si rahisi kuinuka tairi ya mbele pale ambapo utakutana na changamoto ya mlima au mashimo ya barabara.
UBORA..
Boxer ni bora kwani aina ya materials yanayotumika yanaviwango vikubwa kidogo ukilinganisha na sanlg, uliangalia ubora wa chuma cha chasis, ngao inayolinda miguu pamoja na engine, indicators ulikaji wa tairi, bomba la moshi lilipoekwa si rahisi kuunguza mguu hata pikipiki ikikuangukia, ubora wa chain box halipigi kelele mapema n.k ni bora ukilinganisha na sunlg ambayo kama itatokea umepata ajali ni rahisi vitu kama sidemirrows, indicators, dashboard, mikono ya break na crutch kubaki barabarani.
GHARAMA.
Boxer inagharama kwenye manunuzi ya pikipiki yenyewe, vifaa original kama utahitaji kuvifunga pia engine yake inahitaji matunzo zaidi ya maelezo.
sunlg vifaa vyake ni nafuu na engine inavumilia oil hata kama viscosity imepungua mno.
MAJIBU YA SWALI.
engine zote zina nguvu sawa lakini sunlg inaonekana kuwa na nguvu kwa upande wa rough road ama njia yenye milima kama itakuwa na mzigo. na boxer inaonekana kuwa na nguvu katika finaldrive (speed) kama njia ni tambarare na hauna mzigo au mzigo ni wa kawaida.