Ipi inalipa kati ya Reustarant na M Pesa?

Mkuu usiogope, hamna kazi isiyokua na changamoto, na ukikuta kazi inachangamoto nyingi na huko ndo kuna mafanikio makubwa sana, binafsi niko kwenye hiyo biashara mwezi wa nne sasa, namshukuru Allah mambo yanaenda vizuri
IN SH A ALLAH..TUTAJARIBU
 
Humu ndani nawapendea kitu kimoja......kwenye mambo ya maana kama haya mnatoa ushauri mzuri sana na wengine tuna jifunza humu humu...
ila mkiamua siku nyingine mna mpa mtu za usoo....
[emoji23] [emoji23] hakuna km jf for sure
 
Unashangaa nini mkuu? Hiyo ndo gharama za kupata laini ya uwakala wa tigo pesa, mitandao mengine ni bure kabisa
Mkuu imeanza lini?



Na masharti yake lazima uwe na mtaji wa tsh.ngapi?
 
Mkuu imeanza lini?



Na masharti yake lazima uwe na mtaji wa tsh.ngapi?
Siku zote gharama ndo hizo, unachotakiwa kuwa nacho ni leseni ya biashara, tin number na picha 2 za pasport size, baada ya hapo hata 500000 tu unaweza kuanza nayo
 
Unariski vp na ile ni biashara pesa kwa pesa? Biashara ikibuma unaondoka na mtaji wako unaangalia mambo mengine, restaurant, biashara ya viduka vya reja reja ndo pasua kichwa mkuu. All in all location ndo matter
Mkuu wezi wanavamia sana haya maeneo ya m pesa,tigo na airtel money!pia utapeli upo sana mkuu kuhusu hizi biashara jaribu kufuatilia utajua mkuu labda uwe na mtaji kidigo
 
Kuna mtu kanena vyema kwamba biashara yenye faida haikosi changamoto za kutosha.....tatizo letu tunadhani biashara ni capital tu,nitachambua mpesa vs hizo restaurants n shops
MPESA
Hii ni biashara ambayo faida yake inatokana na idadi ya miamala unayofanya kwa mwezi...the more u 0713 728 925 the more commision u get,kwa kuzingatia hili huna budi kuhakikisha kwamba unafungua mpesa eneo ambalo lina flow kubwa ya watu hivo kukuwezesha kufanya miamala mingi zaidi......ili uweze kufanya miamala mingi pia yakupasa kua na mtaji mkubwa sio mtu anakuja kutoa laki5 unaanza kungata vidole,au mtu anataka kueka m1 unatoa macho.
Uzuri wa mpesa/tgo pesa ni kwamba ukiona biashara inasuasua unaweza kuondoka na mtaji wako wote kama ulivo.
Changamoto ya utapeli kwangu haina mashiko kama mhudumu atazingatia misingi ya kazi(simple by checking balance after evry txn)
RESTAURANTS N SHOPS
hizi biashara ni capital intensive kibongobongo....unahitaji viti,vijiko,masufuria,sahani,jiko ,maji mengi,mkaa,gas na majiko yake na zaidi unahitaji watu wa kupika na kusave,vitu vyote hivi vinahitaji pesa kabla hujaanza biashara yako,kwahiyo ikitokea biashara hizi zikafail utajikuta umepoteza karibia nusu ya mtaji wako na stress juu.
Biashara zote zinalipa kikubwa ni ww kujua hizi changamoto na kujiandaa kuzikabili.
 
Umeeleza vizuri mkuu, ni juu ya mhusika kutafakari ni ipi achague kulinga location atakayochagua
 


Uko sahihi kabisa kaka aisee,
 
Anzisha ka-take away kwa mil. 5. Hapo pembeni weka Mpesa n.k. Biashara ya chakula inalipa sana lakini LAZIMA uwe na wapishi wazuri na wahudumu wanaoweza kukaribisha wateja vizuri. Ndio maana nimekuambia uanze na ka take away kenye chips, soda, juice, supu. Wateja wakizidi uingie sasa kwenye vyakula vya restaurant. Lakini uwe na eneo la kutosha ambapo wateja ni wengi kulingana na chakula unachopika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…