Ipi kampuni nzuri ya kuagiza gari kutoka nje kati ya SBT na Befoward?

Hapo inategemea na wewe mwenyewe unachangamka kiasi gani...

Meli ikishaondoka Japan, wanakujuza...zikiisha wiki mbili beforward wanakutumia documents zote za gari kutoka huko Japan kwa kupia DHL au shirika lingine watakalopenda wao...
Ukishakabidhiwa gari lako, unatakiwa kufanya service yeyote au ni kupuyanga tu kwa road?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msaada tena, insurance company wanacalculate vp comprehensive insurance ya gari

Formula ya Comprehensive insurance ni Value of the car * rate jibu utakalopata hapo unazidisha na 18% VAT then unajumlisha na jibu ulilopata mwanzo ndo unapata bei. Kwa mfano thamani ya gari ni 15,000,000 na hiyo kampuni ya insurance unayokata wanatumia rate ya 3.5 maana yake bei ya Comprehensive insurance itakuwa hivi:-
15,000,000 * 3.5% = 525,000

Then:-

525,000 * 18% = 94,500
So bei ya Comprehensive utakayolipia ni:-
525,000 + 94,500 = 619,500
Kwa hiyo kwa gari lenye thamani ya 15,000,000 bei ya Comprehensive insurance itakuwa 619,500 kama hiyo kampuni ya insurance inatumia rate ya 3.5%

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukishakabidhiwa gari lako, unatakiwa kufanya service yeyote au ni kupuyanga tu kwa road?

Sent using Jamii Forums mobile app
Inategemea lipo kwenye hali gani,

Kuna gari lingine linakuja na hali nzuri sana, hapo unaweza kuendesha tu bila shida....kwa sababu haya magari yanakuwa yamekaguliwa kabla hayajaja....ila ukaguzi huu si wakuuamini sana.

Nina rafiki yangu waliagiza vitz ikaja vizuri tu, wakaweka mafuta yakawa yanaisha haraka sana...wakagundua kuwa tank lilikuwa limepasuka.

Lakini inashauriwa umwage injini oil uweke mpya. Pia matairi, unaweza kukuta yamechakaa na yamekaa muda mrefu kwenye barafu huko gari lilipotoka.....hivyo ukiyabadilisha pia ni jambo la usalama zaidi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante sana mkuu
Inategemea lipo kwenye hali gani....
Kuna gari lingine linakuja na hali nzuri sana, hapo unaweza kuendesha tu bila shida....kwa sababu haya magari yanakuwa yamekaguliwa kabla hayajaja....ila ukaguzi huu si wakuuamini sana...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninauzoefu na beforwad...inachukua mwezi na wiki tatu mpaka miezi miwili gari linakuwa limeshafika bandarini....

Wiki tatu mpaka nne za mwanzo ukishalipia gari, wanatumia muda huo kusubiria meli ijae mizigo na taratibu nyinginezo...
Kiongozi vp... uzoef wa kampun ya beforward unao tuwasiliane??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo inategemea na wewe mwenyewe unachangamka kiasi gani...

Meli ikishaondoka Japan, wanakujuza...zikiisha wiki mbili beforward wanakutumia documents zote za gari kutoka huko Japan kwa kupia DHL au shirika lingine watakalopenda wao...
Rekebisho;
Malipo ya TRA yanafanyika mara gari likiingia bandarini,wanalikagua ndio unaandaliwa invoice ya malipo.
 
Inakuaje ukinunua gari kwenye online auction
 
Samahani sijaelewa kidogo Be foward Umenegotiate nao kivipi embu tupe tips kidogo Mkuu !!
Natanguliza shukurani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hapo kwene kubargain apo
i wonder
 
Samahani sijaelewa kidogo Be foward Umenegotiate nao kivipi embu tupe tips kidogo Mkuu !!
Natanguliza shukurani

Sent using Jamii Forums mobile app
Utakapotaka kuagiza gari na Beforward, utatakiwa kufungua account kwenye website yao, moja ya taarifa utakazoweka ni email address yako.

Baada ya kuomba proforma invoice, watakutumia kwa njia ya email, na hapo ndipo mtaanza negotiation. Kwa upande wa SBT, wao hufanya negotiation kwa njia ya simu.

Wao wanakupigia hasa wawakilishi wao wa huku Tanzania.
 
Rekebisho;
Malipo ya TRA yanafanyika mara gari likiingia bandarini,wanalikagua ndio unaandaliwa invoice ya malipo.

Hakuna kitu kama hicho...!!! Malipo ya TRA unafanya pindi unapopokea documents zote za gari lako..!!! Malipo unayofanya gari ikishaingia bandarini ni Port charges ambayo ni malipo ya TPA.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hivi port charge inakuwa fixed? Ni kiasi gani? Pia ukiondoa kodi za TRA ni gharama gani nyingine hapo bandarini?
 
Mmh labda siku hizi..
Ila niliponunua nilipata fursa ya kunegotiate na nilipunguziwa USD 150.

Na gari ya mwanzo nilipunguziwa usd 120 mimi nikakomaa nipunguziwe usd 200....wakakataa kupunguza zaidi...
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…