Kwanza nikwambie kuwa inategemea harusi inayofungwa ni ya dini gani. Mfano madhehebu ya kikristu mengi ukiacha roman catholic (huwa hawajali). Matron wako anatakiwa awe ameolewa..na mume wa huyo matron ndio anatakiwa awe ni patron wa bwana harusi..unatakiwa kuchagua watu ambao watakupa ushauri mzuri na watasimamia maadili ya ndoa yenu kwa ufasaha.
sasa si kila mwanamke anajua kukata mauno na hata kama anajua anaweza asiweze kukufundisha ipasavyo. Ndio maana kuna mtu maalum wa kukufundisha mambo ya chumbani siku ya kitchen party. Na mara nyingi si matron.
Sasa kama kwako wewe ilitokea matron wako akakufundisha si mbaya pia. Mtu yoyote anaruhusiwa kukufundisha. kwa upande wangu sikufundishwa na matron.