Wife mimba yake ilikua na complications nilizunguka karibia hospital zote za kisasa na nishaonana na specialists wengi sana hapa town kila mmoja alikua anashauri anachojua ila kuna siku nimeenda hospital moja nikakutana na dokta wa muhimbili yuko pale part time tukaongea vingi akaniambia afya ni biashara.
Ninachokushauri nakupa rufaa uende muhimbili ukifika nipigie kweli nikafanya ivo kufika nikampigia yule dokta akaelekeza wenzie pale wife akapokelewa kiukweli alipata huduma ya hali ya juu kuliko hata zile private hospital tulizokua tunalipa pesa nyingi licha ya kuwa na bima, madokta walikua wanamuattend kama mke wa mfalme tukaamua clinic ahamie pale hadi siku ya kujifungua.
Kule kwingine walishauri ajifungue wa upasuaji ila muhimbili walisema hamna haja hiyo, kiukweli mke wangu alijifungua salama kwa huduma sawa au zaidi ya zile private nikapata mtoto wa kike na sasa anamiaka miwili mishaanza mawasiloano tena na yule dokta mwakani tukalete mwingine, ushauri wangu hospital za serikali zina huduma nzuri sana kikubwa jenga connection na usiwe na mkono mfupi wapoze madokta na manesi utafurahia huduma yao.