MWAMBA2020
New Member
- Mar 8, 2023
- 2
- 3
Atajifungulia anapofanyia clinic 😄😄😄😄😄Ulitakiwa utwambie Kwaza unakoishi ili utajiwe hospital iliyo jirani
Sio kweli ni moja ya hospital ya ovyo kwa hudumaAcha kupoteza pesa huko,hapo Mombasa uelekeo wa Gongolamboto kuna hospital nzuri tu ya akina mama kujifungua inaitwa CADINAL RUGAMBWA HOSPITAL
Agha Khan kawaida 4 Million.Wakuu habari mimi naomba kufahamu hospitali ipi kwa sasa ni nzuri na ya kisasa kwa mama mjamzito kipindi cha kujifingua kati ya hizi...
Taarifa kama hii ndio anahitaji mleta mada. Bills sio tatizo kwake.Agakhan kama mkwanja upo mpeleke. Mzazi anajifungua kama hajifungui vile uangalizi ni wa hali ya juuu sana kwa mama na mtoto baada ya kujifungua. Ila ka bill karefu
💯wife mimba yake ilikua na complications nilizunguka karibia hospital zote za kisasa na nishaonana na specialists wengi sana hapa town kila mmoja alikua anashauri....
Umetisha[emoji106]Taarifa kama hii ndio anahitaji mleta mada. Bills sio tatizo kwake.
Ulipata huduma nzuri kwa sababu ulipitia kwa mtu shukru Mungu kwa Hilo .Wife mimba yake ilikua na complications nilizunguka karibia hospital zote za kisasa na nishaonana na specialists wengi sana hapa town kila mmoja alikua anashauri anachojua ila kuna siku nimeenda hospital moja nikakutana na dokta wa muhimbili yuko pale part time tukaongea vingi akaniambia afya ni biashara.
Ninachokushauri nakupa rufaa uende muhimbili ukifika nipigie kweli nikafanya ivo kufika nikampigia yule dokta akaelekeza wenzie pale wife akapokelewa kiukweli alipata huduma ya hali ya juu kuliko hata zile private hospital tulizokua tunalipa pesa nyingi licha ya kuwa na bima, madokta walikua wanamuattend kama mke wa mfalme tukaamua clinic ahamie pale hadi siku ya kujifungua.
Kule kwingine walishauri ajifungue wa upasuaji ila muhimbili walisema hamna haja hiyo, kiukweli mke wangu alijifungua salama kwa huduma sawa au zaidi ya zile private nikapata mtoto wa kike na sasa anamiaka miwili mishaanza mawasiloano tena na yule dokta mwakani tukalete mwingine, ushauri wangu hospital za serikali zina huduma nzuri sana kikubwa jenga connection na usiwe na mkono mfupi wapoze madokta na manesi utafurahia huduma yao.
Anajifunguaje peke yake jamani[emoji849]Kama hana pingamizi za uzazi Hata nyumbani tena pekeyake mjamzito anajifungua, kujifungua kwa msaada ni operation tu.
Mpeleke popote tu atahudumiwa, huko ulikotaja mpeleke kama una pesa za kuchezea
Sio tu kupitia kwa mtu mkuu pesa inahusika, bima yangu inacover kila kitu ila nilipaswa kutumia laki kadhaa kujenga mazingira ili kuhamasisha madaktari na manesi ila ilinijengea network naamini next time sitapata ugumu kuwaingia wote niko na namba zao na baadhi hukutana kupata kilaji.Ulipata huduma nzuri kwa sababu ulipitia kwa mtu shukru Mungu kwa Hilo .
Mtoa huduma kazi yake ni kuku monitor tu maendeleo yako, wewe ndio utapush mpka atoke, usidhani utasaidiwa kwa hilo ukishindwa, operation itakuhusuAnajifunguaje peke yake jamani[emoji849]