Ipi ni mechi yako bora ya soka?

Ipi ni mechi yako bora ya soka?

mwehu ndama

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
630
Reaction score
2,151
Nikiwa kijana mdogo kabisa , 30 August 2013 pale Fortuna Arena Czech republic, ilipigwa mechi Kali ya UEFA super cup ,ambayo kwangu ndio mechi Bora ya soka kuwahi kuishuhudia maishani mpaka sasa.

Hii ilikuwa ni baina ya wazee wa BMW , the Bavarian, Fc Bayern munchen dhidi ya wahuni wa London Chelsea FC .

Timu zote mbili zilikuwa katika form ya kutisha sana, Bayern ikiwa chin Pep guardiola Tiktak master , walikuwa wametoka kufungwa na Chelsea msimu mmoja nyuma katika fainal ya UEFA champions league kwa mikwaju ya penalties!.
Huku Chelsea wakiwa chin ya king of low block Jose Mourinho aliyekuwa amerejea klabuni kutoka Real Madrid.

Wakati mchezo ukiwa 2-1 huku Chelsea akiwa anaongoza katika extra time , ndipo pep guardiola anaesifika kwa kusimamia misingi yake ya Tiktak aliamua kuachana nayo na kuamua kuwaruhusu frenck ribery aliyekuwa man of the match , na Arjen Robben watembee wanavyotaka kuelekea golini kwa Chelsea.

Hakika sijawahi kuona Tena maishani mwangu winga za mpira zikitembea kama mafuriko ya maji kama hiyo siku. Ndipo mtangazaji maarufu Peter Drury alisikika akisema "I don’t know how much more of this Chelsea can take! They’re a strong side, no doubt, but right now, they’re hanging on for dear life against this relentless Bayern machine! It’s wave after wave of pure footballing power—how long can they survive this torture?!".

Haikupita muda mrefu Bayern wakasawazisha bao dk 121 na baadae kwenda kushinda kwa penati
 
Mechi yangu bora ni fainal ya Uefa 2014 kati ya R. Madrid vs A. madrid.
R. madrid anakomboa goli dakika ya 94 kupitia kwa mchezaji Ramos inakuwa 1 - 1 anaenda kushinda magoli mengi kwenye extra time.
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    59.3 KB · Views: 1
Manchester city vs real madrid ile game ya nusu fainal second leg iliyoamuliwa na matuta
 
Mechi yangu bora ni fainal ya Uefa 2014 kati ya R. Madrid vs A. madrid.
R. madrid anakomboa goli dakika ya 94 kupitia kwa mchezaji Ramos inakuwa 1 - 1 anaenda kushinda magoli mengi kwenye extra time.
Hii gemu ndio ilimsika rasmi Sergio Ramos legend wa real Madrid..super game
 
Mechi ya chelsea dhidi ya manchester united UEFA fainali 2008 mjini moscow.
 
Hii ni baada ya gem ya kwanza barca kufa chuma nne kule ufaransa .. Neymar alifanya balaah hii gem
Vibaya Mnoo,,Huwaga Kila Nikipata Kijiwasaha Na Nimebahatika Kuwa Na Vijimegabytes Huwaga Naicheki Tena Na Tena Hiyo Gemu,,,Soka Lina Rahaa Na Maajabu Yake Yanayoweza Huzunisha Sana Kwa Upande Mmoja Na Upande Mwingine Furaha Isiyo Kifani Haswa Kwa Matokeo Yake Ambayo Kwa Wakti TofautiTofauti Hustaajabisha.
 
Kombe la Dunia 1998 - France vs Brazil
Kombe la Dunia 2006 - France vs Italy
Kombe la Dunia 2022 + France vs Argentina
 
Mechi ya machester utd vs real madrid pale old Trafford, delima anapiga hatrick, redondo anampita hengingberg kimiujiza miujiza tuu.
Beckham kaingia na kupiga bao. Mechi hatari hiyo.

Nyingine ni fainali ya kombe la dunia la wanawake...usa vs japan. Sii mchezo hiyo mechi ilipigwa mbugi hatari. Japan walikuwa na beki wao mmoja kitasa kweli kweli anaitwa Kumagai 🤣🤣🤣🤣.
Yaani a final worth watching waliolipa hela kucheki hiyo mechi waliburudika sana
 
Mechi ya machester utd vs real madrid pale old Trafford, delima anapiga hatrick, redondo anampita hengingberg kimiujiza miujiza tuu.
Beckham kaingia na kupiga bao. Mechi hatari hiyo.

Nyingine ni fainali ya kombe la dunia la wanawake...usa vs japan. Sii mchezo hiyo mechi ilipigwa mbugi hatari. Japan walikuwa na beki wao mmoja kitasa kweli kweli anaitwa Kumagai 🤣🤣🤣🤣.
Yaani a final worth watching waliolipa hela kucheki hiyo mechi waliburudika sana
Daah Hatrick ya Ronaldo de Lima old Trafford ilikuwa msiba !!hapo man u alitoka kufa 3 -1 barnabeu
 
1. 1998 World cup finals
Brazil ya Ronaldo de Lima Vs France ya. Zinedine Zidane

2. 2023 Ligi kuu Bara
Young africans 5 - 1 deportivo de makolo
(Mechi ya kono la nyani)
Yanga 5 - 1 makolo ndio mechi Bora ya miaka yote soka la bongo..
Ronaldo de Lima el phenomenal, ndie most complete number 9, aliyewahi kutokea duniani, huyu jamaa isingekuwa majeraha nakupenda mbunye angepiga career goals 5000
 
Mechi ya
Brazil vs Egypt 2008 kombe la mabara
France vs Argentina 2022 kombe la Dunia
Liverpool vs Barcelona 2019 semi final UEFA
Senegal vs France 2002 kombe la Dunia
Belgium vs Japan 2018 kombe la dunia
 
Back
Top Bottom