Ipi ni mechi yako bora ya soka?

Ipi ni mechi yako bora ya soka?

Mechi ya
Brazil vs Egypt 2008 kombe la mabara
France vs Argentina 2022 kombe la Dunia
Liverpool vs Barcelona 2019 semi final UEFA
Senegal vs France 2002 kombe la Dunia
Belgium vs Japan 2018 kombe la dunia
Mechi zote dume , kidogo nisahau hii ya mayakuza "Japan "dhidi ya Belgium kudadaki , Belgium walijuwa itakuwa mteremko ,ila mayakuza walikomaa nao mwanzo mwenga ,ila mwisho wa siku mabwanyenye Belgium waliibuka na ushindi wa 3-2
 
Mechi zote dume , kidogo nisahau hii ya mayakuza "Japan "dhidi ya Belgium kudadaki , Belgium walijuwa itakuwa mteremko ,ila mayakuza walikomaa nao mwanzo mwenga ,ila mwisho wa siku mabwanyenye Belgium waliibuka na ushindi wa 3-2
Walijisahau lukaku mtu mbadi
 
Ac Milan vs Liverpool uefa final 2005
Ghana vs Uruguay robo final kombe la Dunia 2010
 
chelsea vs barcelona
goal la tores linaamua mechi hiyo cku nilivurugwa akili
 
1999 Fainali UEFA Champions League.
Dakika 90: Bayern 1-0 Man U

Dakika 93: Bayern 1-2 Man U
 
Mechi ya machester utd vs real madrid pale old Trafford, delima anapiga hatrick, redondo anampita hengingberg kimiujiza miujiza tuu.
Beckham kaingia na kupiga bao. Mechi hatari hiyo.

Nyingine ni fainali ya kombe la dunia la wanawake...usa vs japan. Sii mchezo hiyo mechi ilipigwa mbugi hatari. Japan walikuwa na beki wao mmoja kitasa kweli kweli anaitwa Kumagai
 
1. Fainali ya WC 2022 Argentina Vs France
2. UCL fainali 2006 Arsenal Vs Barca
3. UCL fainal 2008 Man Utd Vs Chelsea
4. Hii ya 4 sitaki ugomvi na makolo ila najua hata wao wanajua
 
Arsenal vs Barcelona moto ulimwagika mpaka sol Campbell aliteguka pua na Barcelona alishinda

Ac Milan vs Liverpool comeback moja ya kibabe mno

Barcelona vs nyumbu aka Manchester United 😀😀😀 ile Barcelona ya kina iniesta mbungi ilipigwa kama vijana wanacheza pes, barca wabaya sana

Germany vs Brazil wale wa Latin America walipigwa kama ngoma 🤓🤓🫡

Spain vs Netherlands game inaisha 1-0
 
Sijui chochote kuhusu mpira.
Ila Nakumbuka kuna kipa kipindi hicho alikuwa anaitwa nyani WA dunia, "anadaka mpaka mishale." Ronaldo de Lima katupia Viwili. Vijana WA njano wanabeba Ndoo ya dunia.
Sijui ilikuwa Mwaka gani huo. Mechi ilikuwa Nzuri, Enzo hizo ka Ronadinho ndiyo kanaibuka.
 
Match yangu bora ni Ile ya BRAZIL vS GERMANY kombe la Dunia 2002 huku DE LEMA kule Oliver khan...
 
1. Fainali ya UEFA Champions League kati ya Manchester United na Bayern Munich iliyochezwa kwenye Dimba la Camp Nou huko Barcelona, Uhispania, tarehe 26 Mei 1999, Mabao ya dakika za majeruhi kutoka kwa Teddy Sheringham na Ole Gunnar Solskjær yalifutilia mbali bao la mapema la Mario Basler na kuipa Manchester United ushindi wa 2-1 na kunyakuwa Ubingwa.


2. Yanga kuibamiza CR Belouizdad kwa mabao 4-0 na kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza. Jumamosi, Februari 24, 2024 kwenye Dimba la Benjamin Mkapa ,Dar es salaam,Tanzania.
Magoli ya Yanga yakifungwa na Mudathir Yahya 43'',Stephane Aziz Ki 46'',Kenedy Musonda 48"' na Joseph Gwede 84''
 
Back
Top Bottom