Ipi ni njia sahihi ya kupaki Gari kwa usalama wa Gear Box

Ipi ni njia sahihi ya kupaki Gari kwa usalama wa Gear Box

mnaongelea magari yakike sio?☹️😕Sisi wa manyu tukutane pale tuelekezane Jinsi yakudrive garizetu zile kwenye foleni halafu uwe leña
 
Wadau hebu tusaidiane kutoana tongotongo. Wengi wetu tumesomea udereva lakini si kila kitu kuhusu gari na matumizi sahihi tunayafahamu. Basi Leo naomba tupeane hints hapa za jinsi ya kupark kiusahihi gari yako hasa hizi za Automatic.

Mimi hufanya hivi siku zote.

Mguu kwenye brake mpaka gari itaposimama kabisa, then Neutral, then na apply Hand-brake, then Parking.

Je, hii ni njia sahihi? Tupeane madini zaidi wakuu
Logic ya kupause kwenye neutral ni ipi?
IMG_20230808_150652.jpg

Mfano mdogo tu ni hiyo chart ya gearbox ya U140E (ipo kwenye rav4, harrier, n. K. )

Imeonesha clutches zipi na brakes zipi zinakuwa engaged au kuwa disengaged kwenye kila gear position.

Sasa zingatia kwenye parking na neutral halafu nioneshe tofauti iko wapi?

Tofautini ni parking pawl tu.
 
Je anayekanyaga Brake mpk gar ikasimama kisha akaweka PArking gear then handbreak.
Je atakuwa sawa au kakosea mpk aanze na handbreak?
Hiyo mnayoita hand brake au parking brake haina uhusiano na gearbox kabisa.

vyovyote utakavyoamua kufanya ni sahihi tu
 
Sio sahihi kwasababu the force point ya gari yako inatakiwa iwe kwenye parking brake na sio parking gear.
Ukipaki gari tambale siyo lazima kuweka parking brake sababu hakuna uzito wowote utakao kuwa kwenye parking pawl.

Halafu hako kachuma(parking pawl) msikachukulie poa, kuna magari mtu anakosa brake(japo ni katika mwendo mdogo anatia parking na gari inasimama na hakakatiki.
 
Asante kwa darasa mkuu, nimejifunza kitu hapa
 
mnaongelea magari yakike sio?☹️😕Sisi wa manyu tukutane pale tuelekezane Jinsi yakudrive garizetu zile kwenye foleni halafu uwe leña
Tujadili namna ya kubalance clutch na mafuta wakati chuma inanyanyukia mlimani 😄
 
Naomba unichanganulie hapa,vipi wakati wa kutaka kuondoka napo inakuwaje,ina maana utapaswa ukanyage brake,then uweke gear kwenye neutral then uachie handbrake au utaondoka kama kawaida?-Hapa nazungumzia kwa gari iliopaki kwenye kilima pua inaangalia bondeni...
Washa weka D au gear #1 halafu ndo ushushe handbrake.
 
Back
Top Bottom