mwanyaluke
JF-Expert Member
- Jan 22, 2015
- 704
- 2,435
Wote tunafamilia tumetokea na wengi tumeunda familia zetu , swali wewe ipi familia yenye kipaumbele kwako inapotokea mgongano wa mambo, hili nauliza kisa rafiki yangu anadai yupo tayari kuvunja ndoa na mke wake kisa mama yake na watoto wa mdogo wake ,ni stori ndefu sana kuisimulia ila kwa mgogoro ulipofika jamaa anatakiwa kuamua abaki na mama au abaki na mke , kubaki na mama anakuwa safe kwenye familia yake, ila watoto wanapoteza haki ya kulelewa na wazazi wote kwa pamoja