Ipi njia bora ya kuachana na mwanamke?

Ipi njia bora ya kuachana na mwanamke?

Azoge Ze Blind Baga

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2019
Posts
442
Reaction score
1,655
Kuna mwanamke nipo nae kwenye mahusiano. Ila kwa sasa sina hisia naye kabisa, natafuta njia nzuri ya kumpiga chini.

Je, nimchane simtaki au nimpotezee kimya kimya, maana anatuma tuma ujumbe kila muda hadi kero?

Wajuvi ipi njia nzuri na ya amani ya kumpiga chini?
 
Njia nzuri ni ile morogoro road ukipitia stendi ya magufuli mbezi mwisho.
Be a man. Hakuna njia nzuri ya kumvunja mtu moyo. We mchane tu kua humtaki abaki abebe msalaba wake wa maumivu.
Nyie wa "njia nzuri" ndo hua mnangojea mkiona amependeza mnaanza kuleta jam ya kurudi kupasha kiporo na maneno ya kienyeji ya kumsingizia shetwani.
Hopeless nigga!
 
Punguza mawasiliano taratibu, kama ana akili ataelewa. Shuleni alifundishwa kuwa "akufukuzae hakuambii Toka".
 
Usimuache, mwambie aijue mipaka yake kama mwanamke tatizo la kumchoka ni kwamba anakutafuta sana yani yuko too desperate. Nakwambia hivi kwa sababu siku akiacha kukutafuta for good ikipita miezi mitatu utamkumbuka alafu istoshe mwanamke ukimuacha anaendaga kua mzuri balaa ili baadae ujutie kumuacha. USIMUACHE ILA MUOMBE SPACE TU.
 
Nilishawahi mwambia ivo manamke nikamuwona anatype kama dk tano ila akaghairi kutuma akapiga kimya nae
 
Usimuache, mwambie aijue mipaka yake kama mwanamke tatizo la kumchoka ni kwamba anakutafuta sana yani yuko too desperate. Nakwambia hivi kwa sababu siku akiacha kukutafuta for good ikipita miezi mitatu utamkumbuka alafu istoshe mwanamke ukimuacha anaendaga kua mzuri balaa ili baadae ujutie kumuacha. USIMUACHE ILA MUOMBE SPACE TU.

Umejuajeee [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Hatufubaiii
 
Back
Top Bottom