Mla Bata
JF-Expert Member
- Jan 24, 2013
- 7,841
- 17,491
Wasalaam,
Hakika Mungu wetu ni mwema nyakati zote, niseme tu mimi Mla Bata si miongoni mwa wafia dini yeyote, wala mwenye kuyajua mengi yahusuyo dini hizi mbili za (ukristo & uislamu), lakini ni mwenye imani ya kuamini kuna nguvu kubwa inayozidi nguvu zote, viumbe vyote na yote yaliyomo ndani na nje ya ulimwengu.
kipindi cha karibuni nilikumbwa na changamoto fulani fulani za kimaisha ziluzonifanya niache kila kitu na nikae chini kusema na nguvu hii kubwa yenye kutawala ulimwengu (Mungu), imani huponya! Mungu amejibu karibia yote niliyomuomba tena kwa kipindi kifupi sana, hivyo kuufanya moyo wangu na nafsi yangu kutamani kufanya jambo kubwa la shukrani litakalofanya niwe na amani,
Nimeshajaribu kwenda kutoa sadaka sehemu za ibada kutoka katika yale niyapatayo kwenye utafutaji wangu, nishatoa kwa wenye uhitaji ikiwemo ndugu na jamaa wa karibu, lakini nafsi yangu haina amani, kila nikikaa nahisi Mungu ananidai shukrani kwa yale aliyonitendea.
Je ni jambo gani la shukrani lenye nguvu linalopaswa kufanywa kama sehemu ya kumshukuru Mungu kwa wema na matendo yake? Kama nilivyosema awali si muumini wa hizi dini mbili za (ukristo na uislamu) lakini naamini kwenye uwepo wa Mungu mmoja mwenye nguvu na mamlaka na ulimwengu na vilivyomo ndani yake, natanguliza shukrani kwa wale wote wenye michango ya kujenga.
Wasalam,
"Everything is possible for those who believe" lets meet at the top, cheers 🥂.
Mla bata
München, Deutschland 🇩🇪.