ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
Nilikuwa naangalia video flani YouTube inahusu capital city za nchi 54 za Africa. Sasa nikaenda sehemu ya comments kusoma nikajionea watu wengi kutoka mataifa mbalimbali dunia wakiisifia Kenya kuwa ndo favourite country yao lakini kiuhalisia ni dhahiri tumewazidi vivutio (Sina haja ya kuvitaja vinajulikana) pamoja na utamaduni tuna makabila mengi ambayo wazungu labda wangetamani kuja kwetu kujifunza Mila za makabila pia tuna amani hatuna historia mbaya ya kumwagana damu kugombana kubwa zaidi tuna eneo kubwa la ardhi mapori yasiyofanyiwa chochote yameachwa tu hivyo ni rahisi kuwekeza tofauti na Kenya ambapo ardhi inashikiliwa na wachache.
Sielewi kwanini wazungu waipende kenya tukisema kwamba sababu ni ina maendeleo sio kweli maana hata kwao ulaya huko wako vizuri tu hawawezi kuja kushangaa magorofa ya Nairobi hapo na hata hivyo kama kutupita kiuchumi hawajatupita sana ni gap fulani la kawaida.
Ingawa pia nilianza kuhisi labda comments hizo zaweza kuwa ni za Wakenya wenyewe wameamua tu kujimwambafy; si mnajua walivyo makanjanja kwenye kujipaisha.
Video yenyewe iko hapo chini search YouTube nenda upande wa comments.