The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,282
- 117,244
Natoka kidooog nje ya maada, nataka kuwakumbusha WAHENGA wenzangu humu; miaka ya katikati ya 80 hasa mwaka 1987 wakati ccm inatimiza miaka 10 ilimletaga mwana muziki wa Kikongo bwana Tabu Ley akiwa na mkewe wa mkataba bibi Mbilia Bel wakiwa ndio wametoka kufunga ndoa yao ndani ya ndege kule Paris France, baada ya hapo band nyingi kutoka Congo/Zaire zilianza kuja kwa wingi nchini mwetu, Pepe Kalle, mzee wa Nzawisa, Kanda Bongoman, Bokilo nk; nakumbuka radio by that time ilikuaga moja tu, RTD (sasa TBC taifa ) na swali ambalo lilikua pendwa sana la waandishi wa habari by that time kwa hawa wana music wa nje lilikua hili, "je umewahi kuusikia music wa Tanzania kabla ya kuja hapa"? Majibu yao yalikua yanafana; kwamba HAPANA sijawahi kuusikia. Binafsi nilikua najiuliza sana why? Wahenga mtakumbuka pia kipindi hicho hicho uliwahi kutokea mgogoro mkubwa sana band ya DDC Mlimani park na radio Tanzania hasa mara baada ya Sikinde kumrudisha mwana music wao kaka Benno Villa Anthon na Maximillian Bushoke kwenye kundi kwamba kazi zao zinauzwa hadi Ujeruman na wao hawapati chochote, ndipo ulipoanza mgogor wa kuto kurekodi pale RTD na badala yake wakaanza kwenda Kenya kabla ya studio ya Don Bosco chini ya MAroon Linje kuanza; now coming back to the question which to me will continue to associate with music industry; nimekua mpenzi sana wa nyimbo hizo za Wakong to date, nasikiliza sana kwa youtube, nasikiliza utunzi wa manguli wa Bongo kina Muhidin Maalimu Gurumo, Bushoke, Hassan rehani Bichuka na solo gita za kina Kassim Mponda, Babu Seya, na yule mashoto wa Ndekule halafu nalinganisha na kina Diblo, Dally Kimoko etc; nakaa najiuliza, why music wetu haukujulikana kama wa Wacokongo/Wazaire those days?? Jibu langu ni rahisi tu, urasimu wa ujamaa na kujitegemea, haukutaka kutangaza chochote nje ya Bongo, tulitaka watu wajue kwa jitihada zao wenyewe which didn't waork out, same same na kwenye UTALII, Kenya inajulikana zaidi kuliko Tanzania ilhali Tanzania kuna vingi kuliko Kenya, makabila as well kama mleta UZI anavyosema, in fact we have a lot compared with Kenya. Tizama hata sasa hivi Kagame anavyoitangaza Rwanda huko majuu; sasa hvi Rwanda inajulikana zaidi kuliko Tanzania; mwanzoni mwa miaka ya 2000 ulikua ukiwa huko nje na kusema unatokea Tanzania, unawaambiwa wenyeji wako kwamba ile nchi ambayo Osama alipiga ubalozi wa Marekani ndio wanaelekewa, nao imeisha pita zaidi ya miaka 20, kizazi kipya kimeingia ambacho wala hakikumbuki about that story of Osama in 1998. Tatizo bado tunao watu wenye mentallity zile zile za kijamaa todate kwenye ulimwengu wa kibepari, angalia hata maofisini kwetu, linganisha utendaji kazi wa Wakenya na sisi, tofauti kabisa. So shida iko hapo kwenye utendaji wetu na kubadirika kulingana na muda, hiyo ndio shida; Kenya ataendelea kusumbua while he/she has nothing comparing with us
Kuna wimbo wa Tanzania unaitwa Dada Asha
Wa Congo waliiba Tanzania...fuatilia history kwanza...hata ule wa Che unapenda dezo Ukaibwa tena na Tshala muana...
Wanamuziki wa Congo wanajua nyimbo zote za Tanzania na wanaiba na kuziimba upya...
Wacongo wanaosema hawajui kuhusu Tanzania waongo...
Tanzania inasimuliwa vizuri huko kwao
Ndo maana wakija hawarudi Hadi wengine tunasahau kuwa ni wacongo kama Dr Remmy Ongala...hujui vizuri history ya muziki Congo na Tanzania