Ipi sababu ya Kenya kupendwa kuliko Tanzania licha ya kuwapita utajiri wa utamaduni?




Kuna wimbo wa Tanzania unaitwa Dada Asha
Wa Congo waliiba Tanzania...fuatilia history kwanza...hata ule wa Che unapenda dezo Ukaibwa tena na Tshala muana...

Wanamuziki wa Congo wanajua nyimbo zote za Tanzania na wanaiba na kuziimba upya...

Wacongo wanaosema hawajui kuhusu Tanzania waongo...
Tanzania inasimuliwa vizuri huko kwao
Ndo maana wakija hawarudi Hadi wengine tunasahau kuwa ni wacongo kama Dr Remmy Ongala...hujui vizuri history ya muziki Congo na Tanzania
 
Wakenya never take sides against their country, wanaipenda nchi yao, wanasifu nchi yao, wanatangaza nchi yao. Watanzania wengi ni vice versa utakuta mtanzania anasema Rwanda ni bora kuliko Tanzania na anashabikia ya hela yote.
muasis sialiufundisha uzalendo au ni porojo tu za madingi zetu
 
Kenya wametuzidi miundombinu, hospitality na marketing strategies
 
RAIS WETU WA AWAMU YA SITA ASIYE NA CHUKI ZA KIMATAIFA WALA KWA MAJIRANI AMESHALIONA HILI NA KAZI AMESHAIANZA,TUWE NA SUBIRA,"KUITANGAZA NCHI IS CONTINUITY WORKS NA SIO KAZI YA ZIMAMOTO,NI SERA THABITI NA MKAKATI THABITI ENDELEVU.
 
Taifa ambalo linakuwa na Marais vichaa ambao hawaamini hata katika kanuni za sheria katika utoaji haki haliwezi kupendwa.
 
Mkuu the Boss heshima kwako; ninakumbuka vizuri sana kuhusu Wakongo hao, nyimbo maarufu (zipo nyingi ) ni mbili, moja ni Tshala Mwana kama ulivyosema, hu uliimbwa na Mkongo aliyekua akiishi Tanzania kaka Ndala Kasheba, mpiga solo pekee ambaye alikua anapiga solo gitaa lenye nyuzi 12 but wimbo huo walifanya makubaliano ya kibiashara, yule mama aliusuka upya na akarekodi na wimbo mwingine wa kaka Shem Kalenga ambaye inaelekea waliwahi kupiga muziki na yule mwizi wake miaka kadhaa nyuma, yule jamaa alikua mpiga rithimu gitaa maalufu wa huko huko Kongo/Zaire, yaelekea yule MKONGO alijua Shem Kalenga aliisha KUFA muda mrefu and hence asingeshtakiwa, na hapa ndipo point yangu ilipo, Shem Kalenga wakati huo alikua anapiga music na band moja ambayo ilikua inapiga show zake nadhani New African hotel wazee wa TUKUNYEMA, now huyu mpiga rithim mkongwe wa Kongo hakua akijua chochote kuhusu music wa Bongo na ndio maana alidhani kwamba Shem Kalenga alikua hayupo duniani, kumbe band yao kila mwaka ilikua ikirekodi RTD album mpya. Sisi tulikua na tatizo, tunalo tatizo hata sasa la kutojitangaza. Just for your information, hadi sasa hivi huko duniani kwenye soko la UTALII, Watalii wengi wanajua Serengeti national park ipo Kenya. Unakumbuka baadhi ya ndege za KQ hadi sasa hivi zimeandikwa Mt Kilimanjaro, imagine, halafu sisi ndege zetu tunaandika "hapa kazi tu" halafu ndege hiyo inakwenda China, imagine!
 
Kwanza Kenya ni famous sana kuliko nchi nyingi za kiafrika hadi nimeona makala na video mbalimbali zinaongelea ni kwanini imekuwa hivyo.
 
wakenya wanajua kujipendeleza na kujishusha. wabongo ni too much know na ujanja ujanja wa kijinga etc
 
Msumari wa Moto huu,wenye ukweli mtupu ndani yake.##tunataka paypal iruhusiwe Tanzania
 
Uganda wanazungumzia zaidi kiingereza kuliko Kenya.
Au Zambia wanazungumza zaidi kiingereza kuliko Kenya. Hebu tutafute sababu nyingine, tuachane na Lugha
 
Lugha gani tena? Hapo umeambiwa nchi 54, au unataka kusema Kenya wanazungumza zaidi kiingereza kuliko Uganda, Zambia, Zimbabwe, ghana, nigeria?
Tutafute sababu halisi
 
Naomba kujua FAIDA ambayo imepatikana TANZANIA kutokana na harakati zake za kisiasa AFRICA ambayo RAIA WA TANZANIA wakawaida anaweza kujuvunia ?

Sent from my SM-G975F using JamiiForums mobile app
 
Wamasai asilia wako kwao
Mlima wa kilimanjaro upo kwao
Na kitambulisho kizuri cha TANZANIA kwa nchi za kigeni useme nchi yako ipo karibu na KENYA ndio utaeleweka.. na viongozi wao sio wababaifu
 
Naomba kujua FAIDA ambayo imepatikana TANZANIA kutokana na harakati zake za kisiasa AFRICA ambayo RAIA WA TANZANIA wakawaida anaweza kujuvunia ?

Sent from my SM-G975F using JamiiForums mobile app
Hakuna faida yoyote nchi ilichopata zaidi ya sifa za kijinga Tu nchi ilikuwa nafasi kubwana kufika mbali kiuchumi Ila Nyerere kwafalsafa zake za uchumi aliididimiza hii nchi Nyerere alichofanikisha kwenye hii nchi ni kuweka umoja WA kitaifa Ila vingine vyote alifeli kama Nyerere angechagua njia moja ya kuinua wananchi wake ambayo ni elimu na kujenga shule nyingi miaka iyoo Leo hii nchii ingekuwa imepiga hatua kubwa sna Ila kulishindwa kujua nini tunataka ashumu mtiani unatungwa mgumu kufelisha wengine ili wafaulu watu wachache sababu ya kuwa na shule chache za sekondari nchini
 
Umeongea kweli tupu πŸ‘ŠπŸΎπŸ‘ŠπŸΎ
 
Comments za hapa haimanishi Kenya inapendwa sana...Huwenda hiyo ndio nchi pekee aliyotembelea Africa sasa atasemaje anaipenda Tz au nchi nyingine kama hajawahi fika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…