Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 4,016
- 6,759
Wajuvi karibuni na wanahistoria tupate elimu. Historia ya kumegwa Kosovo toka Serbia kwa msaada wa NATO na kumegwa kwa CRIMEA&Co(Luhansk,Donetsk,Donbass) kwa msaada wa Urussi.Je umegaji upi ni sahihi na upi ulikuwa Si sahihi?, kwa hoja zipi?.
Ya Ukraine tunayajua, turejee ya Serbia na Kossovo:
Kossovo ilitawaliwa na NATO mwaka 1999 na serikali yake ya muda ya kabila la Albania ilitangaza uhuru wake mwaka 2008, kwa kuungwa mkono na Marekani na washirika wake. Belgrade imekataa kutambua jimbo hilo lililojitenga, na inaungwa mkono na Urusi na Uchina, miongoni mwa zingine.
Baada ya wiki kumi na moja za milipuko ya mabomu katika vita ya 1999, Merika na NATO hatimaye zilishinda vita huko Kosovo. Wanajeshi wa Serbia walilazimika kuondoka, na kuwezesha uwepo wa kijeshi wa kimataifa na kisiasa kuchukua jukumu katika eneo hilo.
Tarehe 9 Juni 1998, Rais wa Marekani Bill Clinton alitangaza "dharura ya kitaifa" (hali ya hatari) kutokana na "tishio lisilo la kawaida na la ajabu kwa usalama wa taifa na sera ya kigeni ya Marekani" iliyowekwa na Yugoslavia na Serbia juu ya Vita vya Kosovo.
Je, NATO imevamia nchi? Watu wanadhani kwamba NATO kama nchi moja kama Ubelgiji kwa mfano, sivyo. inaundwa na nchi 30 wanachama ni muungano wa ulinzi wa pamoja. Ilishiriki katika Afghanistan na Yugoslavia ya zamani
NATO ilishambulia kwa bomu Televisheni ya Redio ya makao makuu ya Serbia na kuua wafanyikazi kumi na sita raia wa Serbia. Hii iliitwa jinai ya kivita na Amnesty International. NATO ilidai kuwa shambulio hilo la bomu lilihalalishwa kwa sababu kituo hicho kilifanya kazi kama chombo cha propaganda kwa utawala wa Milošević.
Ukraine ilikataa kuitambua Kosovo, lakini inaonekana nchi hiyo, ambayo inakabiliwa na vita vya Urusi, imebadili msimamo wake kuhusu suala hilo. Mbunge wa Ukrain, katika majibu kwenye mitandao ya kijamii, ametangaza kwamba amewasilisha Bungeni rasimu ya sheria kuhusu utambuzi wa uhuru wa Kosovo, Oktoba 2022.
Karibuni wanajamvi..
Note😛ro East na Pro West Unazi uje na hoja wa side A na B siyo blah blah