Ipitishwe Sheria ya ukomo wa watoto

doppla2

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2014
Posts
1,363
Reaction score
1,431
Tanzania ni miongoni mwa nchi ambayo fertility rate iko juu sana. Kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2012 kila familia ilikisiwa kuwa na average ya watoto 5.

Takwimu za kiuchumi mara nyingi zimeonya ongezeko la watu nchini haliendani sawa na ukuaji wa uchumi wetu na kusihi mamlaka husika kuchukua hatua mjarabu.

Ziko Sababu nyingi zinazohusishwa kwa nini waafrika wengi hupenda familia kubwa zikiwemo sababu kama watoto ni rasilimali, gharama nafuu ya kuwakuza, na fahari ya uanaume.

Unakuta mzee kazaa watoto zaidi ya 10, huku hali yake ya uchumi hawezi hata kuwahudumia watoto 2, hali inayopelekea watoto kuishi bila msingi mzuri wa malezi.

Na Kutokana na msingi mbovu alioandaliwa na yeye anakuja kupitia hali ile ile na kusababisha kile kinachoitwa vicious circle of poverty.

Kwa msingi huu naona ni Wakati muafaka wa kuja na Sheria ya kudhibiti idadi ya watoto. Mtu ambaye hana akiba ya kutosha ya malezi asiruhusiwe kufyatua tu na kuja kuwapa wengine mzigo wa malezi.

Watu wote wanaolia na umasikini uliokithiri ni waanga wa kutowajibika kwa wazazi wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Japo hoja yako ni nzuri na hoja za kiuchumi kuwa fertility rate yetu ni kubwa kuliko economic growth, lakini kwanza kila mtoto anazaliwa na rizki yake, pili hao wachumi hawajui kuwa soon Tanzania ya viwanda inatupeleka kwenye uchumi wa kati hivyo uchumi wetu utamudu kila family kuwa na watoto 10!. Tumsikilize nani kati yako na rais wetu aliyetuhimiza tufyatue tuu?.

Mimi tayari ninao 8 na bado... namsikiliza rais wetu, sijui nyinyi wenzangu.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…