Dr Restart
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 4,949
- 24,046
Wasalaam.
Baada ya sintofahamu ya baadhi ya Wateule kukataa kuapishwa katika nafasi waliyoteuliwa, kumezuka na maswali na minong'ono mingi isiyo na sababu.
Lakini, yote haya yamesababishwa na kuwepo kwa mawasiliano hafifu baina ya upande wa uteuzi na yule aliyeteuliwa. Kwa akili zangu, nilidhani mhusika hujulishwa kupata nafasi hiyo kabla ya majina kutangazwa hadharani.
Kinachoonekana ni kuwa, mamlaka ya uteuzi yamejitwisha haki ya kuamua hatma ya mteuliwa. Wamesahau kuwa watu wana mipango yao mingi, majukumu yao na wengine hawana mpango wa kushikilia wadhifa za aina hiyo.
Lakini pia, aina hiyo ya uteuzi pasipo kushirikisha pande zote mbili kunaaibisha mamlaka haswa ofisi ya Rais. Mtu kukataa nafasi ya uteuzi ni kuonesha kutokuwa makini kwa wale wote wanaohusika na uteuzi. Na kwa kuwa wateuliwa waliteuliwa na Mh Rais, basi inayoaibika ni ofisi husika.
Kukataa pia nafasi ya uteuzi si jambo geni. Ilishatokea na itatokea tena. Polisi na mamlaka zingine ziheshimu maamuzi ya mtu kwa hiyari. Kuwakamata na kuwahoji kisa tu wamekataa uteuzi, huku wakijua wazi kuwa mhusika ana nafasi nyingine ni kutompa mtu haki ya kujiamulia mambo yake.
Wasaidizi wa Rais kwa hapa wamefeli kwa kiwango kikubwa. Na ingelikuwa vema kama watareconcile na upande mwingine kabla ya kufikia maamuzi ya kuteua.
Nawasilisha.