Ipo haja kwa serikali kupitia maoni, mawazo na matatizo ya wananchi kwa njia ya mitandao

Ipo haja kwa serikali kupitia maoni, mawazo na matatizo ya wananchi kwa njia ya mitandao

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
36,625
Reaction score
89,385
Isiwe kila siku mitandao inachukuliwa kama njia hasi yenye kupinga na kukataa utendaji wa serikali,yapo mengi yanayoweza kusaidia nchi kimaendeleo. Mfano suala la NIDA kuchelewesha vitambulisho nk. wapo wadau wamelalamikia mno na hata wengine kuja na majibu ya nini kifanyike.

Kwa kutumia njia hii kwanza inarahisisha mawasiliano pia gharama za serikali na kuokoa muda. Ni muhimu serikali kuzingatia maoni na taarifa hizi kwani zinatija na wasikariri kila mwananchi anataka nchi yake ididimie, wengine wana mawazo mbadala na yanayofaa.

Ifike hatua viongozi waliangalie hili kwa jicho pevu. Maoni na mawazo yanayopatikana mitandaoni inaongea mengi kuhusu jamii yetu katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Hapa pia intelijensia inaweza kupata taarifa na maoni na kujua matatizo.

Kuna taarifa,maoni na mawazo serikali inachelewa kuzipata na unakuta tatizo au suala husika lilishaelezwa miezi au miaka kadhaa nyuma.

Hapa siwezi hata kuhubiri uzalendo wa nini, hili limeshakuwa taifa kubwa kiana yake cha kufanya ni utekelezaji wa misingi makini,chachu na chungu zinafahamika.
 
Sidhani kama wamekusikia labda ungelieleza hili swala ukiwa TBC ungeeleweka
🙄🙄 Kuna watu hata hawataki kuangalia hiyo channel. !!
 
Back
Top Bottom