Ipo siku Clouds FM itawapigia magoti WCB kukubali yaishe

Wasafi wana Balls! CMG design wameanza sanda mbaya zaidi ngoja tuone 24th itafanzaje
 
Kivipi wakati mmiliki ni mmoja!!?....nyinyi wafuasi ndo mnatoana ngeu yeye anajilia tu!
 
Yani hizi zinaitwa nguvu za soda kama EFM ilivyokuja watu wakasema kwisha Clouds baada ya miaka sasa hadi watu washaanza usiifananishe EFm na WCB.
Huu ni upepo utapita tu na itakua media ya kawaida tu kama ilivyo EFM...
 
Uko sahihi kabisa chief ngoja warukeruke ila watakaa kwenye nafasi yao tu japo mimi sifatilii sana mambo ya sanaa

Kila nikipita kwenye insta naona hao wasafi wanayarudia wanayo fanya CMG huwezi kushindana na alie kufungulia njia labda aamue kukuachia
 
Unailinganisha clouds na wasafi kwa kutumia vigezo gani sasa??

Na watapotezwa kwenye lipi??

Do you think watakuwa na show ya asubuhi kuishinda PB??,,Njia panda,Jahazi,Sport Extra??
kwani wasiweze? kwani wao clouds wamewezaje kuwa na hizo show na wengine washindwe? kuna mtu alijua EATV itapotea?
 
Yani hizi zinaitwa nguvu za soda kama EFM ilivyokuja watu wakasema kwisha Clouds baada ya miaka sasa hadi watu washaanza usiifananishe EFm na WCB.
Huu ni upepo utapita tu na itakua media ya kawaida tu kama ilivyo EFM...
Efm iko vizuri wanafanya vizuri sokoni na kuna baadhi ya vipindi vyao ndo vinaongoza kwa kuwa na wasikilizaji wengi kama "Sports HQ".... Na dhumuni LA Efm siyo kuiangusha clouds no kuleta changamoto kwenye media!... Kama hivi wamegawana wasikilizaji maisha yanaenda!NB:Clouds wamefanya kazi kufika hapo walipo wasafi wanafikiri porojo za kwenye mitandao zitawapush,wajipange kweli!
 
Ndicho ninachosema sasa hivi wako moto kwasababu ya mzuka na madongo mzuka ukiisha watu watasahau kama wanavyosahau matukio muhimu tu
 
Yani Joseph Kusaga ajipigie mwenyewe magoti na kujiambia yaishe??
Kama ni kweli WCB redio ya Kusaga basi utakuta hii tension baina ya Diamond, Ruge na CMG wameitengeneza makusudi ili redio na tv vikick halafu wanakuwa wanatazama wanacheka kabisa jinsi wanavyo control raia kama vile wana human remote control
 
Hizi analysis uchwara tu.
CMG wana contents nzuri sana and they are very creative.
WCB wana michambo sana kwenye social media with very low creativity.

Sasa wewe unesema watampoteza/wamempoteza crouds hata sikulewi, au mbwembwe za wasafi festival kwenye social media ndio zimekuchanganya?
After hizi fiesta na festival kila kitu kitarudi pahala pake, kila mtu atarudi kwenye nafasi yake.

NB; CMG wanahitaji changamoto ili wasiendelee kuwanyonya wasanii, walijimilikisha sana industry.
 
mnachezeshwa kiduku tu hapo...wake up brother. hiyo wasafi ni ya kusaga kama ilivyo clouds...hayo mengine ni mbinu za kibiashara tu.. sana sana atakayepata tabu ni efm! actually sababu za kuanzishwa wcb fm ni efm! CMG ndio baba wa burudani nchini alfa and omega hutaki jinyonge!
 
Ruge yuko wapi kwani?

Ila sioni sababu ya kugombana. Wao ni wasafi festival-Nagwanda, clouds ni Tigo fiesta dar. Sasa kama ni ushindani, wanashindania nini?
 
Ruge yuko wapi kwani?

Ila sioni sababu ya kugombana. Wao ni wasafi festival-Nagwanda, clouds ni Tigo fiesta dar. Sasa kama ni ushindani, wanashindania nini?
Hata mimi nina shangaa japo tarehe ni moja ila matukio yanafanyika mikoa miwili tofauti hata mashabiki hawawezi wagawana
 
Kuna watu wana ujinga mwingi sana. Halafu vyote mi hata sijui fiesta ni nini japo nina miaka mingi naisikia
Hata mimi nina shangaa japo tarehe ni moja ila matukio yanafanyika mikoa miwili tofauti hata mashabiki hawawezi wagawana
 
Kuna watu wana ujinga mwingi sana. Halafu vyote mi hata sijui fiesta ni nini japo nina miaka mingi naisikia
Sijawahi udhuria ila hata mimi sioni mantiki ya kushikana mashati maana ni matukio yanafanyika sehemu tofauti kabisa
 
WCB For Life πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…