Ipo siku tutajenga sanamu ya Hayati Magufuli na kufungua Maktaba yake ili vizazi vijifunze Uzalendo

Soma maelezo acha ushamba alikuwa hawazi kama wew na akili zako ndogo
Wewe umeshindwa hata kujieleza nisome maelezo yapi, ya nani, yaliyo wapi,yenye uhusiano gani na hoja zangu..

Mpaka hapo unajionesha kuwa unaniambia nisome, wakati wewe hujui kuandika.

Nitasomaje?
 
Ni watu wawili wenye IDs ISHIRINII wameajiriwa kumtweza JPM Mtandaoni.

Ni kazi yao, na wanalipwa MSHAHARA.
So kama ni hivyo ina maana wako arobaini, ila mbona humu asilimia 95 hawamkubali huyo shujaa wenu? Na siyo humu tu hata Facebook pia. Wengi wa wanaomkubali huyo shujaa wenu ni Sukuma gang (sina maana ya Wasukuma kama kabila)
 
So kama ni hivyo ina maana wako arobaini, ila mbona humu asilimia 95 hawamkubali huyo shujaa wenu? Na siyo humu tu hata Facebook pia. Wengi wa wanaomkubali huyo shujaa wenu ni Sukuma gang (sina maana ya Wasukuma kama kabila)
SIO KWELI. UKIFUATILIA UTAGUNDUA ID's NYINGI ZA KIMKAKATI ZIMEUNDWA ZAIDI YA ISHIRINI. NI MAKUMI YA IDs.

NA UKIFUATILIA MIANDIKO YAO UNAONA INATOKA KWENYE CHANZO KIMOJA KINACHOFANANA.

KWA MFANO, KILA ID INAYOMTWEZA SHUJAA JPM LAZIMA ITAJE NENO "SHETANI".
 
Hakuna mtu yoyote aliyegusa maisha ya watu iwe kwa mabaya ama mazuri ambaye kumbukumbu zake hazipo. Mpaka leo, kumbukumbu za Hitler, Musolin na hata kina Stalin zipo. Hivyo hakuna jipya hapaa.
 
Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
 
Unaweza toa mfano? Ni unaweza toa mfano wa id ambayo siyo Sukuma gang lakini inamkubali huyo shujaa wenu?
 
Naunga mkono hoja!
Nyerere aliwachukia wabinafsi, wavunja katiba, watu wenye haiba ya umimi ukanda wezi kwa mgongo wa uzalendo wafilisi wabadhilifu watorosha fedha za nchi ughaibuni na wote wa aina hii hawa ni mwiko, na Nyerere alifahamu zaidi jinsi ya kuwaadhibu.
 
Hawa majamaa wanatafuta kulazimisha
Huyo mleta mada si ndiye anatajwa kuwa ni muuaji wa Ben Sanane. Muuaji humwona muuaji aliyemzidi kama shujaa kuliko yeye. Wauaji ndivyo walivyo.

Jambazi humwona jambazi aliyemzidi, kama ndiye shujaa kumzidi.
 
Huyo mtu mwenyewe, kwanza hakuwa msukuma. Huyo kiasili alikuwa ni mtusi wa Burundi. Babu yake na Baba yake walihamia Kigoma tokea Burundi. Kisha wakahamia Sengerema. Marehemu alizaliwa Sengerema. Baada ya kufariki Baba yake, Babu yake, mzee Machalila na wanawe wawili walihamia Biharamulo. Baadaye wakahamia Bukoba. Mzee Machalila alifariki na kuzikwa Bukoba. Mama yake John akaolewa na mume mwingine ambaye alikuwa msukuma. Lakini Magufuli, Baba yake, na mama yake siyo wasukuma.

Na hata angekuwa msukuma, bado siyo sahihi uovu wa mtu mmoja kupachikwa kwa kabila zima. Tufahamu kuwa hata baadhi ya watu ambao marehemu alishirikiana nao kwenye uovu, hawakuwa wasukuma. Akina Sabaya, akina Muro, akina Gambo, hawakuwa wasukuma. Kuna wasukuma wengi tu walioonewa na kuumizwa na marehemu.

Tuwatendee haki wasukuma.
 
Upo sahihi kabisa!mwamba aka chuma kilifanya mambo makubwa sana!!R.I.P CHUMA JPM
 
Mbowe alimuua Ben Saanane na Chacha Wangwe.

Lakini hata hivyo yule Ben Saanane alikuwa na kiherehere sana, alistahili kunyukwa.
Wauaji mnajitokeza wazi. Na ninyi ninlazima mumwone muuaji mwenzenu kama shujaa wa karne.

Ila jambo moja mkumbuke, hamtaipata hiyo nafasi tena. Na kwa uhakika, kadiri siku zinavyoenda uovu wa shujaa wenu na wa kwenu utazidi kuwekwa wazi. Na siku zijazo, watu watatamani hata kaburi lipigwe pingu kama ilivyokuwa wakati wa mkoloni, marehemu akipatikana na hatia, anahukumiwa. Kama umehukumiwa kufungwa miaka 10, mnyororo utafungwa juu ya kaburi kwa miaka 10. Baada ya miaka 10, utafunguliwa kuashiria kuwa umemaliza kifungo.

Huyu hatakuwa tofauti na Stallin aliyeliliwa na mamilioni ya Warusi baada ya kufa. Miaka 13 baadaye, uovu wake uliwekwa wazi, watu wakakasirika, wakaiondoa maiti yake iliyokuwa karibu na maiti ya Lenin, na kwenda kuitupa kusikojulikana.

Itunze hii moyoni: siku zitakavyoenda, ndivyo uovu wa marehemu utakavyozidi kuwekwa wazi na kujulikana kwa wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…