Pre GE2025 Ipo siku yaja kwa huyu mwenezi msipomfunda CCM na Rais Samia mtavuna mabua

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Vita ya kugombea madaraka itawaua.
 
Hii tabia ya kutatua kero majukwaani wala sio utendaji sahihi. Mara nyingi umelenga kujitafutia sifa kwa raia wasio na uelewa. Mkuu wa wilaya unakuta ana kero 50 mezani mwake amezitatua 30 na nyingine zipo kwenye mchakato.

Anakuja mwenezi, anatajiwa kero moja pale jukwaani, anafoka foka na kuitatua anapata ma marks kibao. Naungana na mtoa mada kuwa mwenezi akichekewa ataanza kumpinga hata rais indirect. Maana kuna vi kauli anatamka live kuwa angekuwepo JPM ningefanya hivi, tatizo mama ni mpole. Hiyo kauli ki falsafa sio sifa ni kuponda kiana.

Akichekewa, ipo siku mtoto atamtamkia mama kuwa usinizingue, kwanza naweza kukuzaa. Wapenda sifa huwa wanawinda jamii ya watu wa chini waliofail kimaisha ambao akili za uchambuzi wa kauli za viongozi hawana. Mwenezi kwa sasa anaogopeka kuliko mama. Ipo siku kichwa kitazidi mwili, maana wazee walisema, "Ndama huzaliwa na masikio, baadaye ndo pembe zinaota." Nahisi pembe za mwenezi zipo speed kwenye uotaji wake.
 
Mama angalia kwa umakini huyo mwenezi wateule wako wameanza kumuogopa wamekuachia wewe so be carefull mama yetu.

Falsafa yako ya uongozi imelenga kuongoza nchi kwa kufanya kila raia ajisikie amani kujiita mtanzania.
JPM alikuwa aggressive sana kiasi kwamba hata mahusiano ya kimataifa yalikaa vibaya maana alikuwa anatumia resources zake zote na hata muda mwingine kutumia uhuni na uongo ili afanikishe adhima yake.

Kumbuka JPM walimpenda sana watu wa chini ambao furaha yao kuona tajiri wa mtaani kwao nae akishushwa wanahisi wanapata ahueni ya maisha ndo maana akijiita RAIS WA WANYONGE. Masikini na jealous ni tako na mavi i mean vipo jirani.
 
sijui kwanini nafsi yangu inapata furaha na amani nikiona masisiemu yanaparurana na kujazana hofu wao kwa wao?. hii kitu mpaka leo sijapata jibu lake.
 
Mkuu umemwaga nyongo
 
 
Wewe ni mgeni wa siasa,unataka kusema kuwa wewe ndo unauelewa mkubwa ndani ya CCM kuliko waliompa cheo comredi Makonda!?. Kwamba bossi wa comredi Makonda hajui lolote juu ya sliyemteua?


Ni ngumu sana kumuelewa Makonda,kaa kwa kutulia ,acha awanyooshe,huwezi vumilis Option ni moja tu, hama chama!
 
Tanzania yetu
Tanzania na Afrika inamuhita MTU aina ya Makonda.
Makonda ni Joshua Wa Tanzania.
Hatutaki Vibaraka Wa Wazungu na waarabu wakamilishe Lengo Lao la kuuza Nchi.
Makonda ni mfano Wa Kuigwa.

Hii Nchi imevamiwa na kuporwa na Wageni Kila Kona .
Viwanda vya sukari zaidí ya Kumi Halafu sukari Bei Juu.
Tatizo ni nini .
Mabasi yapo mpaka special Hire Halafu Latra wanapandisha Bei Wakati Wa Krismass.walikua wanamnuafisha Nani na wanamkoma Nani Kama sio Mtanzania maskini.

Polisi na wanajeshi wanastaafu wanalipa pensheni kama mshahara mmoja Wa Mbunge na Waziri Halafu wanawaambia wajiandae kuwashughulikia wapinzanai kwenye Uchaguzi.
Wanasiasa ndani ya CCM ni wanafiki sana.
Paulo Makonda ndiye atakayeijenga CCM kwenye kizazi hiki kinachotamani Mapinduzi ya Kijeshi Ili Nchi iongozwe Kwa usawa Kwa Wote kufuata Sheria Kwa nguvu kubwa na kuwatiumua Wezi na wavamizi Wa Taifa hili waliojificha ndani ya CCM na kupewa madaraka makubwa.
Wanapora Mali za watanzania wanakimbizia ndugu Zao huko wanakotoka .

Makonda Hata akianzisha Chama chake anawashinda Wanasiasa Wote wabinafsi na wahuni.

Makonda ni kijjana makini sana kwenye siasa za Kiafrika.
Angekua nje ya mfumo angefaa sana kujiunga na Mwabukusi na Heche na Lisu na kuunda chama chao.

Kama Wananchi hasa vijana wenye nguvu wanamkubali Makonda na wapo tayari kwenda Naye Hao Wachache wanaolinda maslahi Yao Kwa unafiki Hawana cha kumfanya.
Vijana makini wapo ndani ya mifumo ya kiusalama na wanajua uimara na Umakini Wa Paulo Makonda. Hakuna Mtanzania anayelitakia mema na usalama Wa Taifa hili anayempinga Makonda.

Wanaomchukia Makonda ni madalali Wa Wahuni Toka nje na wanaangulia maslahi Yao na SIO usalama ,uimara na maendeleo ya Wananchi Wote.

Makonda Chapa Kazi.
Mama anakuamini na anajua unaweza kufanya kazi nzuri na 2025 CCM ikashinda.
CCM SIO MTU mmoja ni Chama cha wakulima na Wafanyakazi . Wakulima na Wafanyakazi wengi wanaodhulumiwa Haki zao wapo na Makonda kukijenga chama.
 
Aisee
 
Kwa hiyo makonda anatufaa zaid kuliko hao
 
Kwa hiyo makonda anatufaa zaid kuliko hao
Anatufaa sana mana pakiwa na Katiba ya mfumo Wa kifalme panahitaji usimamizi na maamuzi magumu ili kujenga nidhamu.

Katiba yetu haitoi nafasi Kwa wateule kuwajibishwa na MTU mwingene yeyote isipokua Rais au kufuata misingi ya Chama kushika hatamu na maelekezo ya vikao vya CCM.

Kwa Hali ilivyo Hata Tume ya Maadili ya Uongozi na PCCB wapo Kama kichaka tu cha ajira na mishahara mikubwa lakini havina nguvu Juu ya wateule Wa Rais.

Sasa akitokea MTU Wa kumpa Rais Taarifa za kweli na za wazi basi tumlinde sana mana Hii Nchi inaliwa Kwa speed kubwa sana na wanasiasa na familia Zao hasa Rais anapokua mpole na mwenye Huruma Kama Mama.

Tuchukulie mfano wewe Ukiwa na saiti Yako ya ujenzi Halafu wasimamizi na mafundi wakawa wanaiba sementi,nondo na vifaa vingine huku wakijenga Kwa kiwango cha chini; Halafu ukampata kijana mwenye uwezo Wa kuwadhibiti na kuwakemea Hao mafundi wahuni utawasikiliza wale wanaolalamika kuwa wanafokewa na kudhibitiwa au utafurahi kumpata msimamizi mzuri na jasiri.
 
Hili nililisema tangu zamani kwamba Makonda ni timu Sukuma Gang na kwamba baada ya kupenya kuingia uongozini, ataanza mchakato wa kumuangusha mama kupitia chawa wengi wa kundi hili waliomo serikalini. Ikifika 2025 tayari kundi hili litakuwa limeota mizizi ya kutosha. Halitaweza kurudishwa nyuma wala kutishwa kwa vyovyote vile na timu ya mama.

Sasa ni wakati muafaka timu ya mama imshughulikie mapema kiongozi huyu wa Sukuma Gang kabla hajaleta madhara kwa chama, serikali na kundi la mama. Wasipoziba ufa mapema, watakuja kujenga ukuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…