Pre GE2025 Ipo siku yaja kwa huyu mwenezi msipomfunda CCM na Rais Samia mtavuna mabua

Pre GE2025 Ipo siku yaja kwa huyu mwenezi msipomfunda CCM na Rais Samia mtavuna mabua

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mama angalia kwa umakini huyo mwenezi wateule wako wameanza kumuogopa wamekuachia wewe so be carefull mama yetu.
Falsafa yako ya uongozi imelenga kuongoza nchi kwa kufanya kila raia ajisikie amani kujiita mtanzania.
JPM alikuwa aggressive sana kiasi kwamba hata mahusiano ya kimataifa yalikaa vibaya maana alikuwa anatumia resources zake zote na hata muda mwingine kutumia uhuni na uongo ili afanikishe adhima yake.
Kumbuka JPM walimpenda sana watu wa chini ambao furaha yao kuona tajiri wa mtaani kwao nae akishushwa wanahisi wanapata ahueni ya maisha ndo maana akijiita RAIS WA WANYONGE.Masikini na jealous ni tako na mavi i mean vipo jirani.
Duh sasa nijisikie amani kujiita mtanzania kwa lipi mkuu katika hii nchi?
 
Duh! Kwa hiyo,wafanyakazi serikalini wabembelezwe kufanya kazi zao? Wakijisikia walale,mwisho wa mwezi walipwe.
Kwa nini wafanye kazi kwa woga? Wakitimiza wajibu wao,nani atawafatilia kuwawajibisha!?
Suala la nidhamu ya hiari limefeli sasa si bora wawe na nidhamu ya uoga tu.
 
Sidhani kama ulimaanisha
Anatufaa sana mana pakiwa na Katiba ya mfumo Wa kifalme panahitaji usimamizi na maamuzi magumu ili kujenga nidhamu.
Katiba yetu haitoi nafasi Kwa wateule kuwajibishwa na MTU mwingene yeyote isipokua Rais au kufuata misingi ya Chama kushika hatamu na maelekezo ya vikao vya CCM.
Kwa Hali ilivyo Hata Tume ya Maadili ya Uongozi na PCCB wapo Kama kichaka tu cha ajira na mishahara mikubwa lakini havina nguvu Juu ya wateule Wa Rais.
Sasa akitokea MTU Wa kumpa Rais Taarifa za kweli na za wazi basi tumlinde sana mana Hii Nchi inaliwa Kwa speed kubwa sana na wanasiasa na familia Zao hasa Rais anapokua mpole na mwenye Huruma Kama Mama.


Tuchukulie mfano wewe Ukiwa na saiti Yako ya ujenzi Halafu wasimamizi na mafundi wakawa wanaiba sementi,nondo na vifaa vingine huku wakijenga Kwa kiwango cha chini; Halafu ukampata kijana mwenye uwezo Wa kuwadhibiti na kuwakemea Hao mafundi wahuni utawasikiliza wale wanaolalamika kuwa wanafokewa na kudhibitiwa au utafurahi kumpata msimamizi mzuri na jasiri.
Tuombe Mungu,na iwe hivo kama ulvotolea huo mfano.
 
Hili nililisema tangu zamani kwamba Makonda ni timu Sukuma Gang na kwamba baada ya kupenya kuingia uongozini, ataanza mchakato wa kumuangusha mama kupitia chawa wengi wa kundi hili waliomo serikalini. Ikifika 2025 tayari kundi hili litakuwa limeota mizizi ya kutosha. Halitaweza kurudishwa nyuma wala kutishwa kwa vyovyote vile na timu ya mama.

Sasa ni wakati muafaka timu ya mama imshughulikie mapema kiongozi huyu wa Sukuma Gang kabla hajaleta madhara kwa chama, serikali na kundi la mama. Wasipoziba ufa mapema, watakuja kujenga ukuta.
Sidhan, mwenezi hafanyi Kwa ajil ya hilo gang, he is working for His own empire.
 
Haujui unachokitaka: unampinga mwenezi halafu unamalizia kuomba utatuzi wa anayoyapigania mwenezi!

Huyu ndiyo tunamtaka kwasasa na si kesho. Anayemchukia ni mjinga na mwenye ajenda zake za Siri. Unamchukia vipi mtu Tena kiongozi wa chama tu aliyejitoa kutetea na kutatua kero za wananchi Tena wanyonge. Rais kashindwa,makamu kashindwa,waziri mkuu kashindwa,naibu waziri mkuu kashindwa,mawaziri wameshindwa,naibu waziri wameshindwa,wakuu wa mikoa wameshindwa,wakuu wa wilaya wameshindwa,RAS,DAS hovyo tu. Usidhani kama sisi ni wajinga kujaa kwenye mikutano yake. Ana kitu huyu kijana na anafaa kwasasa kwani amesaidia watu wengi mno. Vipi kama angekuwa na mamlaka ya kikatiba sasa? Go makonda gooooo!
Hakika,Inabidi tumpe mamlaka kamili
 
Lakin saa inakuja,nayo sasa ipo,ambapo mtavuna mnachokipanda, kwa jicho la mbali mnamuona kama anakijenga chama, katika jicho la upeo wa roho anadhoofisha chama, bosi wake na Viongozi wakuu wengne na kujijenga yeye.

Anajisafisha na kujitanabaisha alikuwa ni mtu mwema, kiongozi shupavu na jasiri. Mpaka sasa anamuheshimu mwendazake na ndiye bosi wake wa moyo wa mda wote. Ndo mana anaishi falsafa zake na ndio anazohubiri, falsafa hizo zinalengo la kuwaibua wale walompenda na kufanya aonekane yeye ndo mrithi sahihi, Wale walompenda Mwendazake sasa watampenda huyu kwa heshima na kweli na watamuimba kama shujaa wao na hakuna atakae weza kuzuia.

Mama Falsafa yako ilitanabaisha watumishi wa serikali wasifanye kazi kwa woga, bali kwa weledi na nidhamu,ila falsafa inayohubiria majukwaani kwa sasa ni hofu na umaarufu wa mtu.kwa vile watumishi wengi wa serikali ni waoga, wamejengwa kuogopa wanasiasa,zile zama za woga zinarudi, na hakika watumishi na wateule wako wote wanamuogopa huyu kuliko kiongozi yeyote ktkt taifa hili, huku akijijenga kwa wale wananchi mnaowaita walalahoi na wanyonge wamuone ndiye kiongozi pekee mwenye udhubutu na kukemea maovu.

Hakika nakwambia ,watanzania wanataka kiongozi anayesema na kutenda, anayeonya na kukemea kweli kweli, anayewajibisha watumishi wa umma wazembe na wabadhirifu wa mali za umma na hii ndio beat anayotembea nayo Mwenezi.
Asipofundwa vizuri atakufarakanisha na wale uliokuwa umeanza kupatana nao,haki uliyoitengeneza na kuipigania itapotea. Mhe raisi binafsi naamini unafanya kazi nzuri sana na nakupenda kwa dhati kwa sababu unapenda haki na usawa kwa wote lakin nakuomba usiamni sana hawa wasaidizi wako,wengi wao wanaangalia vyeo na matumbo yao,usiwakumbatie sana kana kwamba bila wao nchi haitaenda,kuna wateule wako wanakuharbia halafu wanakusifia wakiamn utafurahishwa na hizo sifa.maagizo yako hawayatekelezi kabisa na wanafanya yao kwa mgongo wako.

Ole wenu msipotafta namna ya kumfunda, ipo siku yaja hamtaweza kuyazuia mafuriko, Kama lengo ni kumjenga kuwa kiongozi basi ni vema mkamjenga sawasawa kwa sababu kama atabadilika ni kiongozi mwenye udhubutu na huenda akaleta Mabadiliko katika nchi, anahulka ya kupenda Maisha ya kifahari lakini anachukia wengine wanaoyaishi, anapenda mamlka na kuamuru lkn hapendi anayemzidi mamlaka, anapenda kusaidia watu na anataka ajitanabaishe ni yeye pekee mwenye huruma na moyo wa kusidia watu, anapenda kuonekana ni mcha Mungu kuliko wanaosimama madhabahuni.

Maisha yameguwa magumu sana mtaani,Mama sekta bnafsi zinazofanya kazi na serikali hasa zinazolipwa na pesa kutoka HAZINA hazilipwi kwa wakati na kusababisha baadhi kuzorota au kufa hasa za wazawa,umeme umekuwa ni tatizo na kero kubwa sana kwa wananchi,watu wanategemea umeme kufanya shughuli zao zinazowaingizia kipato na kuendesha Maisha yao lkn umeme umekuwa ukikatika kila uchao jambo linalowafanya wananchi kuanza kuchukia serikali.zaidi Viongozi wa serikali wengi hasa wateule wako wanaishi Maisha ya kifahari na bila shaka kero ya umeme kwao haiwapati

Iwe jumapili njema kwenu,Maandiko yanasema ‘basi sasa msiwe watu wa kudharau,vifungo vyenu msije vikakazwa,maana nimeskia kwa Bwana,Bwana wa majeshi,Habari ya hukumu itakayotimizwa,nayo imekusudiwa.
Makonda kaachiwa nchi Mama anaswampa ughaibuni akirudi anakuwa kizi city na kuondokea huko kurudi ughaibuni.....nchi haina mwenye uchungu nayo....Jeshi linalalamika Rais analalamika....mamlaka zinalalamika wana chi wanalia na kulalamika
 
Huyu ndiyo tunamtaka kwasasa na si kesho. Anayemchukia ni mjinga na mwenye ajenda zake za Siri. Unamchukia vipi mtu Tena kiongozi wa chama tu aliyejitoa kutetea na kutatua kero za wananchi Tena wanyonge. Rais kashindwa,makamu kashindwa,waziri mkuu kashindwa,naibu waziri mkuu kashindwa,mawaziri wameshindwa,naibu waziri wameshindwa,wakuu wa mikoa wameshindwa,wakuu wa wilaya wameshindwa,RAS,DAS hovyo tu. Usidhani kama sisi ni wajinga kujaa kwenye mikutano yake. Ana kitu huyu kijana na anafaa kwasasa kwani amesaidia watu wengi mno. Vipi kama angekuwa na mamlaka ya kikatiba sasa? Go makonda gooooo!
Naunga Mkono hoja....

Kwa kweli akisimama 2025, CCM watakuwa na kazi nyepesi sana maana Watanzania wengi (ukiondoa mafisadi wachache na yenye nguvu ya fedha), tunawapenda watu kama Paul C. Makonda.

Hii ni kwa kuwa watendaji wetu hawana uzalendo wala uadilifu wa kufanya pasipo kusimamiwa.
Makonda ni msimiaji mzuri sana.

Kama hatokuwa Rais 2025, basi apewe hata Uwaziri Mkuu.
Naiona Tanzania mpya chini ya Makonda..
 
Hata Kama ni mtu Miaka 64 ni Mingi Hata akili Itakuwa imeanza kuchoka na kupungua uwezo wa kufikiria na kukabili changamoto .
Miaka 62 sio mingi au hapo akili itakuwa haijanza kupungua na kuchoka?Najua unajua namzungumzia nani.Au kipimo hicho ni baadhi ya watu tu?

Ingekuwa kisayansi uwezo wa akili unapungua tusingekuwa na viongozi wenye umri zaidi ya huo duniani.
 
Hakuwa anazungumzia issue za Makonda bana...mbona kwa Makonda alijibu vizuri..acheni kugombanisha
Hiyo ni clip ya muda mrefu kuhusu bei elekezi ya mazao.Haina uhusiano wowote na ziara ya Makonda.Ukiona watu wameanza kutetemeka jua kuna linalowatetemesha.
 
Back
Top Bottom