Pre GE2025 Ipo siku yaja kwa huyu mwenezi msipomfunda CCM na Rais Samia mtavuna mabua

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Duh! Kwa hiyo,wafanyakazi serikalini wabembelezwe kufanya kazi zao? Wakijisikia walale,mwisho wa mwezi walipwe.
Kwa nini wafanye kazi kwa woga? Wakitimiza wajibu wao,nani atawafatilia kuwawajibisha!?
Kwani makonda ndiye mkuu wa divisheni/idara zote za serikali? Huko wanakofanya kazi hawo watumishi wa umma hakuna wakuu wao wanaowaongoza kutimiza majukumu yao au unataka kusema nini mkuu?
 

Hakuna tatizo kwa wanaCCM wenye uwezo kujitokeza kugombea na Mama Samia 2025. Mama hakugombea kile kiti. Alikipata kwa bahati nzuri tu. Sasa anatakiwa apitie mchakato wa kugombea urais kwenye nchi yenye watu milioni 61, lakini haina uwezo wa kukusanya kodi na kuendesha nchi kwa pesa za ndani zaidi ya kutegemea misaada inayokuja na masharti ama ya ushoga, ugaidi, na itikadi zisizofaa kwenye nchi hii kwa usalama wa wananchi wote kwa na vizazi vijavyo.

Hatutaki kumpa mtu yeyote nchi kwa bahati. Mtu asimame aseme nini maono yake kwa Watanzania wote. Mtu atuambie nini kinachosababisha umaskini wa kitaifa wakati kuna wachache waliopo kwenye madaraka wanaogelea kwenye mali kutokana na madili ya kuhujumu nchi. Atapambana vipi na wahujumu uchumi kwa kutumia katiba iliyopo endapo hana mpango wa kuleta katiba mpya? Je, katiba iliyopo ataitumia vipi kupambana na ufisadi wakati taasisi zote hazina meno ya kuwang'ata na kuwakemea wateule ambao ndio wafujaji wa mali za umma?

Wagombee wengi kutoka makundi mbalimbali watuambie kwa nini kodi zinaongezeka kwa kasi na mikopo kila siku, lakini matumizi na starehe kwa watawala yanakwenda juu na wao hawajali? Nini watafanya kwa kutumia katiba hii ya kidikteta bila kutawala kwa misingi ya kuwafukuza na kuwakemea wezi?

Atuambie ni kwa nini alisema katiba ni kijitabu tu kisicho na nguvu wakati ndicho kinachompa nguvu na kuyafanya majeshi yenye nguvu kumtii kwa misingi ya kijitabu hicho hicho?

Aliyepo muda wake unaisha 2025 kwa msingi wa uteuzi wake ndani ya Chama 2015 hadi 2025. Wajitokeze wengine wagombee kushindanisha serikali na maono. Historia ya dunia inaonyesha kuwa dunia inaleta mabadiliko kutokana na maono ya mtu mmoja na sio chama, wala wanachama, wala makundi ya watu.

Musa, Yesu, na Muhammad ni mtu mmoja aliyeibadili dunia kwa maono yake na misingi aliyoiamini. Kwa sasa, aliyepo yupo pale kwa sababu ya umakamu wa rais 2015-2025.
 
Mama yenu mwenyewe kampigia simu Makonda LIVE mkutanoni huko Moshi juzi tu na kusema anamuunga mkono kwenye huo ufuatiliaji wa utekelezaji wa ILANI ya chama na kusikiliza kero za wananchi.

Ndiyo maana hutokaa umsikie tena Nchimbi wala Kinana akipiga vijembe anachokifanya Konda,hapo tayari kaamua kiutu uzima.

Actually,hiki anachokifanya Konda ndiyo watz wengi wanakitaka, uwajibikaji nchi hii kwa sasa ni sifuri huko maofisini.
 
Rais anahitaji msaada gani?! Huyo Makonda sasa anatoa msaada gani Kwa Rais?
 
Kwani makonda ndiye mkuu wa divisheni/idara zote za serikali? Huko wanakofanya kazi hawo watumishi wa umma hakuna wakuu wao wanaowaongoza kutimiza majukumu yao au unataka kusema nini mkuu?
1. Mimi nimeongelea aliesema woga wa wafanyakazi kuwajibishwa.
2. Nadhani kila kitengo kina mkubwa wa kuwajibishwa, na pia nadhani kuna njia sahihi ya kuwajibishwa kisheria.

Labda kwao hawanaga wakubwa! Pengine hata kwa umri wake na anaowaajibisha, alitakiwa apunguze kasi.
Ila sasa, kama katumwa, afanyeje?
 
Mleta mada kuna wimbo wa Bob Marley unaitwa "Who cap fit, let them wear it."

Kwenye huu wimbo kuna maneno yanasema

"Who Jah/God bless, you can't curse him".

Makonda ana kila dalili za kuwa mtu aliyebarikiwa sana sana.

Makonda amepitia majaribu na vigingi vya kutosha ila hadi sasa ameviruka.

Kama kwa Miaka 2 alipokuwa nje ya siasa hakuna aliyeweza kumdhuru fikiria atakuwa amebarikiwa kiasi gani
 
Huyu ndiyo tunamtaka kwasasa na si kesho. Anayemchukia ni mjinga na mwenye ajenda zake za siri. Unamchukia vipi mtu, tena kiongozi wa chama tu aliyejitoa kutetea na kutatua kero za wananchi, tena wanyonge. Rais kashindwa, makamu kashindwa, waziri mkuu kashindwa, naibu waziri mkuu kashindwa, mawaziri wameshindwa, naibu waziri wameshindwa, wakuu wa mikoa wameshindwa, wakuu wa wilaya wameshindwa, RAS, DAS hovyo tu. Usidhani kama sisi ni wajinga kujaa kwenye mikutano yake. Ana kitu huyu kijana na anafaa kwasasa kwani amesaidia watu wengi mno. Vipi kama angekuwa na mamlaka ya kikatiba sasa? Go Makonda gooooo!
 
Maisha ni kutesa kwa zamu. Mwaka huu na ninyi mnaisoma namba. Hapo mnapesa na kila kitu lakini hamna amani kisa kijana wawatu anapendwa na watanzania.
 
Mara ngapi? Sisi huku ni shangwe tuu muache azidi kuharibu

Sent using Jamii Forums mobile app
Anaharibu wapi, acheni kudanganya watu nyie... Msimtishe Mh Rais wetu bila sababu. Mnadhani wenyewe hamjui vizuri. Tatizo, bana, mafisadi yakishaona kuna hali ya hatari, yanaanza kujitengenezea barrier ya kutoguswa. Hata kama anatembelea nyota na Magufuli, kuna tatizo gani? Wakati katika nyota ile, hata mama yetu Dr SSH alikuwemo. Mmeshaona chama kinajirekebisha na kuwa kikali, mmeanza kulialia. Wacha watu wachape kazi, iwe lolote lakini wananchi wanahitaji matokeo: maji, umeme, bei nafuu, mfumuko wa bei chini, mafuta chini, sukari chini, n.k. Sijui unaelewa. Hayo mengine ni propaganda zako za kutunga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…