Inajulikana Mengi na watangazaji/wanahabari wao wengi ni supporters wa Yanga. Lakini, hawajui wanajiharibia biashara? Nakumbuka walishawahi kufanya hivyo miaka ya nyuma na wasikilizaji na watazamaji wanapenda michezo wengi waligeukia vyombo vingine vya habari.
Siyo mambo ya visasi, watangazaji na waandishi wa habari na wapiga picha wa ITV walizuiliwa na uongozi na mashabiki wa simba kuingia uwanjani kuonyesha mechi yao na kutangaza. Si wameona kuwa Dar ndiyo kuna mashabiki tu? Viongozi wetu wa vilabu hawajumlishi na kutoa kabla hawajafanya maamuzi hasa hawa akina Kaduguda..kampuni za IPP zinaendeshwa kwa visasi, yaani thinking yao ni kama watoto wadogo. hata kama ni kweli some few Simba people walileta mzozo na crew ya Itv is it fair kuwanyima habari wanaSimba waliojaa nchi nzima?? sijawahi kuwaona watu wanafiki kama IPP Media, to hell with them....
Hii hoja haina ukweli na haihusiani na mzozo uliopo kati ya Simba na vyombo vya IPP. Unataka kuniambia Mengi ameanza kuishabikia Yanga juzi wakati mechi na Lyon/Manyema, mbona kabla ya hapo habari za Simba zilikuwa zinaandikwa na kutangazwa katika vyombo vya IPP? Tuache unafiki, swala lipo wazi ni kweli Simba walikuwa na haki ya kuja haki yao ipo wapi mechi yao ikirushwa live, lakini approach yao ni ya kimtaani mtaani zaidi, ilikuwa ni suala la wao kuwasiliana na TFF na sio kutishia kuvunja vifaa ya kurushia matangazo. Huo ni UHUNI!
Mkuu uko sahihi kabisa,approach ya simba ilkuwa ya kimtaani zaidi na IPP walijitetea kuwa walishapata baraka za TFF.
Walichotakiwa kufanya ni kwenda TFF kujua haki yao wanaipata vipi lakini si kutishia kuvunja vifaa vya kurushia matangazi live.
Hatoendelee ngo mpaka dunia inakwisha tutabaki na uswahili wetu!!
magehema umenena ukweli mtupu,kama wanazi wa simba waliona wanakosa haki yao wangefata taratibu kupitia tff wakajua watapataje haki yao,sio kuleta mambo ya kihuni nakuanza fujo nakutaka kuvunja vifaa vya kazi wanajua thamani yake,ni mapesa mengi mno kuvinunua,mm binafsi nawaunga mkono waandishi wa ipp kuwasusia simba wako sawa kabisa.Hii hoja haina ukweli na haihusiani na mzozo uliopo kati ya Simba na vyombo vya IPP. Unataka kuniambia Mengi ameanza kuishabikia Yanga juzi wakati mechi na Lyon/Manyema, mbona kabla ya hapo habari za Simba zilikuwa zinaandikwa na kutangazwa katika vyombo vya IPP? Tuache unafiki, swala lipo wazi ni kweli Simba walikuwa na haki ya kuja haki yao ipo wapi mechi yao ikirushwa live, lakini approach yao ni ya kimtaani mtaani zaidi, ilikuwa ni suala la wao kuwasiliana na TFF na sio kutishia kuvunja vifaa ya kurushia matangazo. Huo ni UHUNI!
Kama mtu amekufukuza utafanyaje?Shida ni kwamba IPP Media inongozwa na kwa mkono wa chuma! Mengi ni ka dikteta kadogo, yaani jamaa hajambo kwa visasi! Uki-mess naye utakuandama, tabia za kitoto sana hizo! Wanafanya migogoro kuwa personal na sijui hata hana mshauri! Hivi ukikataa kutangaza habari za simba nani ana-loose! Kama nilitaka kuona matokeo si Nitaenda Channel 10, au Star TV. Simba hawana cha kupoteza ila wao ndio itawa-cost!
Pili IPP sio ya Mengi ni ya Watanzania wanao invest na wewe unapata faida unapowanyima haki yao ya kupata news kwa sababu ya ugonmv wako na Simba, that is too person! na inaonyesha hata upeo wako wa kuona mbali ni mdogo kwa sababu wewe unawaona simba tu lakini Big picture umemyima haki kila mtanzania ambaye hata hajui unachogombania!
Ni kweli kabisa Mkuu...Inajulikana Mengi na watangazaji/wanahabari wao wengi ni supporters wa Yanga. Lakini, hawajui wanajiharibia biashara? Nakumbuka walishawahi kufanya hivyo miaka ya nyuma na wasikilizaji na watazamaji wanapenda michezo wengi waligeukia vyombo vingine vya habari.
IPP ilisha wahi kususia kutangaza habari za Yanga? kwani nini simba tu...acha wasi tangaze tutasikiliza TBC,Clouse FM, RFA na nk au nawao wamegoma maana dagaa alidundwa na FFU mpaka akalazwa vipi haandiki taarifa za michezo siku hizi!?...Siku hizi vyombo vya habari kibao wakisusa JF si ipo!?...teh tehKama mtu amekufukuza utafanyaje?
Ukivunja chombo cha mamilioni ya fedha utamdai nani wakati viongozi wa simba na mashabiki wao ni waganga njaa (mimi ni shabiki wa simba). Hakuna ugomvi kati ya IPP na Simba bali walikataa mechi isiyonyeshwe na waandishi walizuliwa na ilikuwa mtafaruku hata vyombo vingi vya habari vilitangaza hiyo kimbwanga. Sasa kama TFF walitoa kibali na wanachama wake wanakataa au wanaleta fujo na TFF iliyotoa kibali haijachukua hatua yoyote, sasa chombo cha habari kingefanyeje?
Hapo watakapoona umuhimu wa kutangazwa watakwenda mezani wenyewe kusema sasa hatutawapiga uwanjani na kuwekeana mikataba ya maelewano.