IQ

Husninyo

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2010
Posts
23,851
Reaction score
9,472
Hivi IQ ya mtu inapimwa vipi?

Unajuaje kama huyo mtu au mtoto ana IQ kubwa au ndogo?
 
Mwekee vitufe viwili vyenye rangi za bluu na kingine cha kijani...akichukua Kijani jua huna mtoto!
 
IQ ina vipimo vyake vya kitaalamu, so kama unataka kuestablish kiwango halisi cha IQ yako au ya mwanao au ya mtu mwingine, waone wataalamu mahospitalini hasa wa masuala ya afya ya akili. IQ ikiwa sawasawa ni nzuri, ikiwa kubwa ni nzuri zaidi ila ikiwa ndogo sana si nzuri na ikipungua au ikizidi kwango kinachotakiwa basi huleta matatizo ya akili. baadhi ya watoto wanaoanza kuonyesha wana mtindio wa ubongo toka utotoni pamoja na wale watundu kupita kiasi, huwa ni kwa sababu ya IQ kubwa! siku hizi kuna utaalamu wa kumanage IQs kwa hiyo ukiwahi matibabu, kuna uwezekano wa kuicontrol at some levels
 
Website mbalimbali zinatoa simple IQ tests ambapo utaweza kujua IQ yako. Just google IQ tests.
 

barikiwa miss jud. Nimekuelewa vizuri.
 
Husninyo, kwa mtazamo wangu hivi vipimo vya IQ sio accurate, yaani vinaweza kukupa general picture, lakini sio acurate. Kwa vipi?

Kwa sababu, vingi vyao vipo kwa kiingereza, na hata maswali yake huwa yanalenga jamii ya kiingereza. Kwa hiyo ukimfanya mtanzania anayeongea kiswahili huwa sio rahisi kupass ukizingatia na mmarekani anayeongea kiingereza.

Karibia IQ test zote zilizopo online zipo kwa kiingereza na zinakuwa na maswali ambayo ni rahisi kujibu kama umekulia kwenye jamii ya kiingereza. Kwa hiyo unaweza kufail swali tu kwa sababu hujaelewa linauliza nini, na sio kwa kuwa we ni mjinga.

Mi mpaka leo sijaona universal IQ test ambayo haipo language-based au culture-based.

kwa hiyo usizichukulie serious sana hizi tests.
 
Hizi IQ Tests huwa zinanishangaza. Asilimia kubwa ya maswali yamekaa kihesabu hesabu.. Kujua Hesabu inategemea na mapenzi ya mtu kwa somo hilo, Binafsi sipendi Hesabu. Kunipima IQ yangu kwa kutumia Hesabu ambayo siipendi siyo fair.. Wakati mwingine inakuwa ngumu kushawishi mtu kwamba hiki kitu ni valid..
 
kwa hiyo ndugu IQ yako ni ndogo
 
Sioni kama ni vibaya kama utafanya research kwenye website yoyote inahusiana na IQ TEST na pia unaweza ukaonana na Psychologists ili kujua ni vipi unaweza ukaipima IQ na ukatujulisha na sisi wote pia wa hapa JF

nitafanya hivyo mkuu.
Ahsante.
 

kuna mwalimu wangu alikuwa ananiambia ukielewa hesabu ujue na masomo mengine pia rahisi kuyaelewa.
 

nimekuelewa mheshimiwa.
 
Hizi online IQ test ni sawa na mchezo wa watoto kwa jamii fulani na kamwe sidhani kama ni kitu cha kugundua uwezo wako wa kiakili au kufikiria kwani zinauliza maswali ambayo nadhani hayana uhusiano wowote kuwa mtu akishindwa kujibu ni mbumbumbu!
 
kwa hiyo ndugu IQ yako ni ndogo

Possible.

kuna mwalimu wangu alikuwa ananiambia ukielewa hesabu ujue na masomo mengine pia rahisi kuyaelewa.

Kujua kitu mara nyingi huenda sambamba na kuwa na mapenzi juu ya kitu husika, kwa mfano mimi nilianza kuichukia hesabu tangu niko form two kwa sababu ya mwalimu wake (akili za utotoni), nikaamua kuiweka pembeni, na bado nikawa nafaulu kwa kiwango cha juu masomo mengine. Bado siashawishika kukubali kwamba kutumia hesabu kupima IQ ya mtu kama njia sahihi (au labda napinga kwa sababu IQ yangu ndogo kuweza kuelewa? LOL)....
 

Lakini hesabu zinazotumika kwenye kupima IQ ni hesabu ndogo ndogo tu ambazo watu wengi bila kujali umri wanaziweza, yaani mtoto wa miaka 10, au mzee wa miaka 75 wanakuwa wanaziweza. Hebu fikiria mfano huu:
Una dose ya dawa vidonge vitatu, unatakiwa kunywa kila baada ya nusu saa. Je utamaliza dose baada ya muda gani?

Sasa ukiwa kilaza utazidisha nusu saa mara 3 upate jibu dakika 90 (saa moja na nusu) na hapo ni kwamba IQ yako ina mushkel
Lakini ukiwa kichwa, utapata jibu sahihi la dakika 60 (saa moja) mara moja.
 
hahahahahaha....... yani wewe ndo huna akili kabisa kwamba mtoto akichagua kijani ujue anawaza kuchakachua tu.............hahaha:decision:
Haaaaah!!! Kumbe ndio maana yake...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…