Revolution
JF-Expert Member
- Feb 28, 2008
- 960
- 927
Husninyo, kwa mtazamo wangu hivi vipimo vya IQ sio accurate, yaani vinaweza kukupa general picture, lakini sio acurate. Kwa vipi?
Kwa sababu, vingi vyao vipo kwa kiingereza, na hata maswali yake huwa yanalenga jamii ya kiingereza. Kwa hiyo ukimfanya mtanzania anayeongea kiswahili huwa sio rahisi kupass ukizingatia na mmarekani anayeongea kiingereza.
Karibia IQ test zote zilizopo online zipo kwa kiingereza na zinakuwa na maswali ambayo ni rahisi kujibu kama umekulia kwenye jamii ya kiingereza. Kwa hiyo unaweza kufail swali tu kwa sababu hujaelewa linauliza nini, na sio kwa kuwa we ni mjinga.
Mi mpaka leo sijaona universal IQ test ambayo haipo language-based au culture-based.
kwa hiyo usizichukulie serious sana hizi tests.
Mojawapo ya njia ni kuangalia mtu anayeargue vizuri kama huyu jamaa niliyemquote, yeye ana IQ kubwa kwa kuwa ameargue vizuri na mimi nina IQ kubwa kwasababu nimeweza kumgundua kwamba ana IQ kubwa.