Lyambalyetu
JF-Expert Member
- Apr 6, 2021
- 278
- 255
Iramba imebahatika sana baada ya Uchaguzi wa Mwaka jana 2020.
Katika mkoa wa Singida kama sikosei ni Iramba pekee iliyotoa mawaziri.
Tuna Waziri Dr. Mwigulu Nchemba, Prof. Kitila Mkumbo (ingawa wa Ubungo wana haki naye pia) na Dr. Dorothy Gwajima.
Mwenyezi Mungu abarikiwe sana sana! Tuna bahati sisi.
Mkoa wetu pia kama sikosei una Naibu Katibu Mkuu mmoja - yule wa Afya Dr. Jingu kama sikosei. Kama wapo wengine mtanisaidia, lakini katika yote Iramba imebarikiwa.
Pamoja na Baraka hizo - Mbunge hasa hasa anayewakilisha Iramba - Dr. Mwigulu Nchemba haonekani kama atakuwa na manufaa kwa Iramba - amejiimarisha kitaifa zaidi hasa pengine kutokana na ambitions zake za kuutaka URais.
Dr. Mwigulu amejikita zaidi kwenye siasa za Kitaifa badala ya kuangalia maendeleo yetu.
Kwa kifupi ni ushauri wangu kuwa Dr. Mwigulu sasa, pamoja na nafasi ya Uwaziri wa Fedha aliyonayo, aangalie zaidi Jimbo lake la Iramba.
Kwa sasa anatumika awamu ya tatu ya ubunge wake na Mwaka 2025 atakuwa katumikia miaka 15. Katika miaka kumi iliyopita hana ambacho anaweza sema amekifanya kwa Iramba kinaweza kukumbukwa.
Akimaliza miaka 15 katika status hii kama ya leo basi ili kuongeza miaka mingine 5 Mwaka 2025 ajiandae kuiba kura kama alivyofanya 2025.
Lakini akumbuke kuwa kutumainia kuiba kura Mwaka 2025 kunaweza kumtokea puani. JPM hayupo na mission alizokuwa akitumia JPM zinaweza zisiwepo 2025.