kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,846
- 20,319
Iran na Uturuki zahimizwa kuunganisha nguvu zao kupambana na Marekani
Mkuu wa chama cha Vatan cha Uturuki amesema kwamba kuna wajibu kwa Ankara na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuunganisha pamoja nguvu zao kupambana na vikwazo vya Marekani dhidi ya nchi hizo mbili.
Dogu Perinçek amesema hayo leo na kuongeza kuwa, Iran ni mshirika wa kiistratijia na ni jirani mwaminifu kama ambavyo ndiyo nchi inayoidhaminia Uturuki sehemu kubwa ya mahitaji yake ya nishati na ni kwa sababu hiyo ndio maana ushirikiano wa Ankara na Tehran ukawa ni jambo la dharura na muhimu sana katika kukabiliana na ubeberu wa Marekani.
Mkuu huyo wa chama cha Vatan cha Uturuki ameongeza kuwa, ushirikiano wa kiistratijia baina ya Tehran na Ankara na ushirikiano mzuri wa nchi hizo mbili katika suala la Syria, bila ya shaka yoyote ni jibu thabiti kwa vitisho vya Marekani.
Vile vile amesema, serikali ya Uturuki inapaswa kuachana mara moja na siasa za kuipiga vita Syria na badala yake ifanye juhudi za kurejea uhusiano na kutoa mkono wa urafiki kwa Damascus kama njia ya kuimarisha ushirikiano uliopo hivi sasa baina ya China, Russia na Iran.
Hivi karibuni Marekani iliziwekea vikwazo vya kidhulma Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uturuki ikiwa ni kuzidi kuwathibitishia walimwengu ubeberu wake.
MY TAKE: NAONA UTURUKI ASHAANZA KUJITOA TARATIBU UPANDE WA MAGHARIBI JUZI KAOMBA AUNGWE KWENYE KUNDI LA BRICS