Naona Mwawado umesepa...Lol...au bado una google?
Hapana Mkuu "sijakwepa" nafikiri ulimaanisha hivi,maana "kusepa" napata wasiwasi kinaweza kuwa sio kiswahili,lakini nimekuelewa ulikuwa unamaanisha nini.Ndugu yangu nilipotea kidogo shughuli zilikuwa nyingi na kwa bahati mbaya sikuikumbuka hii thread mpaka nilipoona Mwanzange amejibu leo....naomba fuatilia majibu yangu kwa uchache kama ninavyofahamu/fuatilia kutoka vyanzo mbali mbali vya habari,lakini pia nipo wazi kukosolewa kwa yale ambayo hautokubaliana nayo...kidogo muda umekuwa tatizo kwangu,lakini najua kuna Wanachama wengine wanaweza kukupa majibu hapa.
Swali:Kwa nini Obama anaweza kuwa ni Tough Kuliko Viongozi Wengi waliomtangulia?
Katika kipindi chake kifupi cha Utawala ameweza kufanya mambo mengi kama ifuatavyo:
1;Mapema Mwezi wa April/2009 Utawala wa Obama Uliondoa Vikwazo vya kusafiri kwa Wamarekani kwenda CUBA na wanaendelea na Mazungumzo na Utawala wa Raul kwa nia ya kuondoa Vikwazo vya Uchumi/Biashara ambavyo vimedumu kwa miaka 48 sasa.
2;Utawala wa Obama umefanikiwa kurudisha uhusiano wa Kidiplomasia na Utawala wa caracus (Venezuela).Rais Hugo Chavez aliuomba Utawala wa Obama umrudishe Balozi wa US aliyefukuzwa Caracus sept/2008,kwa madai ya kuwasaidia Wapinzani wa Serikali na kutaka kumuua Rais Chavez.Utawala wa Chavez uliomba kurudisha uhusiano wa kibalozi baada ya Marais hao wawili kukutana na kusalimiana Mjini Trinidad Tobago.
3;Utawala wa Obama kwa kupitia Wizara ya mambo ya nje, mwezi May/2009 umeweza kuwashauri Wa-Iran na kumuachia Mwanahabari Roxana Saberi ambaye alihukumiwa kwenda Jela kwa kosa la Ujasusi.
4;Wanahabari Laura Ling na Euna Lee waliachiwa huru baada ya Rais Clinton kutumwa na Ikulu ya US kwenda kuuomba Utawala wa North Korea kuwaachia wanahabari hao kwa sababu za kibinadamu.Wanahabari hao walivuka mpaka kutoka China bila kufuata taratibu za uhamiaji.Kwa kosa hilo walihukumiwa Nchini Korea Kaskazini, kifungo na kazi Ngumu.
5;Rais Obama amerudia tena ahadi yake ya kufunga Gereza la Guantanamo huko CUBA.Gereza hilo ambalo linalalamikiwa na Jumuiya za kimataifa kama ndio mfano wa kukiukwa kwa Haki za Binadamu.Toka Januari 2009 mpaka sasa wafungwa 250 wamekwishatolewa hukumu, kutokana na kesi hizo Wafungwa hao wapo kwenye Magereza mbalimbali Duniani na ndani ya US,kati ya hao wafungwa 75 wameachiwa huru kwa kukosa ushahidi wa kuwatia hatiani.Gereza la Guantano litafungwa kabisa kabla ya Februari/2010.
6;Katika Ziara yake Moscow Julai iliyopita,Rais Obama akishirikiana na Rais Medvedev waliweza kutia saini kupunguza silaha kali za kinyuklia kutoka wastani wa makombora 6000 mpaka 1000 kwa kila upande (USA/Russia),punguzo hilo litaendelea taratibu mpaka kiwango cha kila upande kutokuwa na kombora lolote.Pia USA iliahidi kusimamisha shughuli ktk kituo chake cha kudaka Makombora kilichopo Nchini Poland,na kusimamisha shughuli ya kituo cha kuona/ kugundua (Radar station) makombora kilichojengwa Nchini Czech.Kwa asilimia kubwa ziara ya Obama Nchini Russia imetafsiriwa kama ziara ya mafanikio na inayofungua upya ukurasa wa ushirikiano.
7;Ili kuhimiza Utawala bora,State Department imetoa majina ya baadhi ya Viongozi wanaotuhumiwa kwa Ufisadi na kuhusishwa na vurugu katika Uchaguzi Mkuu Nchini Kenya.Miongoni mwa Viongozi hao 15 wamenyimwa viza ya kuingia Nchini Marekani,ambako walikuwa wanafuatana na Waziri Mkuu kuja kwenye Mkutano wa 64 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa.Utawala wa Obama umekuwa unalaumu viongozi wengi wa Kiafrika kwa kujilimbikizia mali na kutojali maendeleo ya watu wake.
8;Kwa mara ya kwanza Rais Obama katika Baraza kuu la UN alimwambia Waziri Mkuu wa Israel waache kabisa kuongeza majengo/makazi huko Gaza na kwenye maeneo ya Judea na samaria,maneno hayo makali hayajawahi kuzungumzwa na Rais yeyote wa USA.Rais pia alimuonya Rais Abas kwa kusema kuwa "mashambulizi ya makombora yanayofanywa na Hamas ni lazima yakomeshwe ili turudi kwenye Meza ya majadiliano".
9;Kwa mara ya kwanza Rais Obama ametofautiana na Makamanda wake wa Jeshi kwa kukataa kuongeza Jeshi Nchini Afghanistan mpaka aelezwe kwa kina Mkakati wa kuwepo kwa Jeshi kubwa Nchini Afghanistan.Rais ambaye alikuwa anafikiri ni vyema kupeleka Wafanyakazi wengi Raia kutoka State Department kuliko Askari kwa maana ya kwamba,kinachohitajika huko si vita bali ni mikakati ya kuijenga Afghanistan katika sekta za Elimu,Huduma za Jamii,Maendeleo ya wanawake,na Elimu ya Uraia.Suala la vita na kung'oa mizizi ya Extremists ni suala la serikali ya Karzai zaidi kuliko serikali ya USA.Bado kuna mazungumzo marefu kabla ya uamuzi wa kuongeza Askari kufikiwa mwishoni mwa oktoba.kuna Wafanyakazi 800 wa State Department Nchini Afganistan.
Hizo ni sababu chache tu...za siasa za ndani na Nje ambazo zinaweza kuonyesha ni kiasi gani Obama ni Tough katika maamuzi mbalimbali.