Iran yakana huhusika kwenye shambulio la Salman Rushdie. Yasema Rushdie na wafuasi wake ndiyo walaani na kukemea tukio hili

Iran yakana huhusika kwenye shambulio la Salman Rushdie. Yasema Rushdie na wafuasi wake ndiyo walaani na kukemea tukio hili

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Zikiwa zimepita siku mbili tangu Salman Rushdie ashambuliwe kwa kuchomwa kisu sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kulazwa chumba cha wagonjwa mahututi huko Marekani, msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya Iran Nasser Kanaani amefutilia mbali madai yanayoendelea kushika kasi kuwa serikali ya nchi hiyo imehusika kwenye shambulio lililolenga kutoa uhai wa mwandishi huyo wa kitabu cha Aya za shetani.

"Kuhusu shambulio la Salman Rushdie huko Marekani, hatudhani kama kuna yeyote anayepaswa kukemewa, kulaumiwa au hata kulaaniwa kwa kufanya kitendo hiki isipokuwa yeye mwenyewe (Salman Rushdie) na wafuasi wake.

Salman Rushdie (75) alishambuliwa ijumaa ya august 12,2022 huko New York, Marekani, wakati akijiandaa kutoa hutuba kwenye hadhara moja. Kwa mujibu wa wakala wake, sehemu kubwa ya ini,mkono pamoja na mishipa ya fahamu ya Rushdie ilijeruhiwa vibaya na upo uwezekano mkubwa wa kupoteza jicho moja.

Sehemu nyingine ya maelezo ya Kanaani inasema kuwa hakuna mtu anayeweza kuilaumu Iran kwa namna yoyote ile kwa kuwa imejipambanua kutokuhusika kwenye tukio hili. Aidha, inaamini kuwa matusi na kejeli alizozitoa pamoja na uungwaji mkono aliopata lvilikuwa ni tusi kubwa kwa dini zote.

Kwa miaka zaidi ya 30, Rushdie amekuwa anaishi chini ya vitisho vya kifo baada ya kutoa andiko lenye kichwa cha habari "AYA ZA KISHETANI" lililoleta hisia hasi kwa waumini wa dini ya kiislamu, hali iliyofanya kiongozi mkuu wa nchi ya Iran Ayatollah Ruhollah Khomeini atoe fatwa inayohalalisha kifo chake.

KIjana aliyehusika kwenye shambulio hili Hadi Matar (24) amekana kuhusika kwake kupitia kwa mwanasheria anaye msimamia.

Hali ya Salman Rushdie kwa sasa imeanza kuimarika, anaweza kupumua pasipo usaidizi wa vifaa maalumu.

Chanzo: ABC NEWS
 
bora wamekana mapema maana sasa hivi Marekani amefura kama Koboko.
backup za iran zote now zinachezeshwa sindimba
sisi wavaa kobazi wafuasi wa ayatola tunakusupport
kana baba.
 
Back
Top Bottom