Iran yakubali kufungua mlango Bahari wa Hormuz kwa muda wa wiki mbili

Iran yakubali kufungua mlango Bahari wa Hormuz kwa muda wa wiki mbili

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Abbas Araghchi, ametangaza kuwa Iran itakubali kusitisha mapigano na Marekani “ikiwa mashambulizi dhidi ya Iran yatasitishwa”.

1775627312161.png
Aliongeza kusema kuwa “kwa kipindi cha wiki mbili, usafiri salama kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz utafunguliwa”.

Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, ambaye amekuwa akisimamia mazungumzo kati ya Iran na Marekani, amesema kuwa usitishaji huo wa mapigano umeanza kutekelezwa mara moja.

1775627695765.png
Naye Rais Donald Trump wa Marekani amesema uamuzi huu kwa Marekani ni "ushindi kamili" baada ya makubaliana ya kusitisha vita kwa wiki mbili na Iran.

Soma: Trump asitisha shambulio zito dhidi ya Iran dakika za mwisho! Vita kusitishwa kwa Wiki mbili. Nini kinaendelea na nani Mshindi?

Katika mahojiano na Agence France Presse baada ya tangazo lake, alisema kwamba Iran "itajadiliwa kikamilifu" chini ya makubaliano hayo.

"Vinginevyo nisingekubali," Trump alisema, bila kutoa maelezo yoyote kuhusu kile ambacho kingetokea kwa urani.

Israel inaunga mkono uamuzi wa Rais Trump wa kusimamisha mashambulizi dhidi ya Iran kwa wiki mbili kwa makubaliano ya Iran kufungua mara moja Mlango Bahari na kusimamisha mashambulizi yote dhidi ya Marekani, Israel na katika nchi za eneo hilo.
 
Back
Top Bottom