Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Iran imerudisha dozi 820,000 za chanjo ya virusi vya corona iliyotolewa kama msaada na Poland kwa sababu ilitengenezwa Marekani.
Televisheni ya taifa siku ya Jumatatu ilimnukuu Mohammad Hashemi, afisa wa wizara ya afya, akisema kwamba Poland ilitoa takriban dozi milioni moja za chanjo ya AstraZeneca ya Uingereza na Uswidi kwa Iran.
"Lakini chanjo zilipofika Iran, tuligundua kuwa dozi 820,000 kati ya hizo ambazo ziliagizwa kutoka Poland zilitoka Marekani," alisema.
Waziri wa afya wa Iran, Bahram Einollahi, aliandika katika barua kwa mkuu wa mamlaka ya forodha kwamba licha ya uhakikisho wa Poland,chanjo hizo zilitoka kutoka "chanzo kisichoidhinishwa".
Alisema watoa huduma wa Poland wameahidi "kubadilisha chanjo hizo na zile kutoka kwa chanzo kilichoidhinishwa" na kurudisha chanjo zilizorejeshwa.
Mnamo 2020, Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Hosseini Khamenei, ambaye ndiye mwenye usemi wa mwisho juu ya maswala yote ya serikali, alikataa uwezekano wowote wa chanjo za Marekani au Uingereza kuingia nchini, na kuziita "haramu".
Iran sasa inaagiza tu chanjo za Magharibi ambazo hazijazalishwa Marekani au Uingereza.