Sheria mpya inayopendekezwa nchini Iraq inayolenga kupunguza umri wa ridhaa ya Ndoa kwa Wanawake hadi miaka tisa, jambo linalolenga kuruhusu Wanaume Nchini humo kuoa Wanawake wakiwa na Umri mdogo
imepingwa vikali na Wanaharakati Nchini humo wakidai kuwa ni yenye kuhalalisha udhalilishaji wa kijinsia kwa Watoto ambapo pia inaelezwa kuwa Sheria hii inataka kufuta moja ya sheria bora zaidi za haki za Wanawake katika Mashariki ya Kati, ambayo inawapa Wanawake haki za kudai talaka, malezi ya Watoto, na urithi.
Wanaharakati na baadhi ya Wabunge wa Iraq wanapinga kwa nguvu pendekezo hili, wakisema kuwa litakuwa janga kwa haki za Wanawake na Watoto, Raya Faiq, ambaumye ni Mratibu wa Makundi ya kupinga sheria hii, alisema kuwa pendekezo hili litaruhusu Ndoa za Watoto na kuminya haki za Familia za kukataa Ndoa hizo huku akiweka wazi kwamba sheria hii ingekuwa ni njia ya kisheria ya kuruhusu udhalilishaji wa kijinsia kwa Watoto.
Pia, soma: Bunge la Iraq lajadili mpango wa kuruhusu ndoa za utotoni, kushusha umri wa mabinti kuolewa hadi miaka 9
Aidha Serikali ya Iraq, kwa upande wake, inadai kuwa mabadiliko haya yatasaidia kufuata sheria za Kiislamu, wakisema kwamba yatawalinda Wasichana kutoka kwa mahusiano yasiyofaa lakini hata hivyo, Wanaharakati wanasisitiza kwamba sheria hii itawarudisha nyuma Wanawake na Watoto kwa miaka mingi.
Sheria hii ilipitishwa kwa mara ya pili Bungeni mnamo Septemba 16, 2024, na inatarajiwa kupitishwa tena kutokana na msaada kutoka Vyama vya Shia Nchini humo lakini hata hivyo inaelezwa si Vyama vyote vya Shia vinaunga mkono sheria hii, na bado kuna juhudi kubwa za kupinga.
Mapambano haya ni muhimu kwa Wanawake wa Iraq, ambao wanapinga vikali hatua hii, wakiitaka Serikali kuepuka kurejesha nyuma haki za msingi za Wanawake na Watoto.