Irene Ombeni Mwanadada anayefanya ufasi kwa kujitolea apatiwa vifaa vya usafi na Mbunge

Irene Ombeni Mwanadada anayefanya ufasi kwa kujitolea apatiwa vifaa vya usafi na Mbunge

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,455
Reaction score
5,134
Screenshot 2026-10-16 at 16-04-53 Instagram.png

Screenshot 2026-10-16 at 16-05-14 Instagram.png

Screenshot 2026-10-16 at 16-05-39 Instagram.png

Screenshot 2026-10-16 at 16-06-01 Instagram.png
Baada ya kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Tv kumfungulia dunia Kijana ๐—œ๐—ฟ๐—ฒ๐—ป๐—ฒ ๐—ข๐—บ๐—ฏ๐—ฒ๐—ป๐—ถ kwa kufanya nae mahojiano na jamii kuona anachokifanya, Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Mhe. ๐—›๐—ฎ๐—ฟ๐—ฎ๐—ป ๐—ฆ๐—ฎ๐—ป๐—ด๐—ฎ (haransanga_) amemuwezesha Mwanadada Kijana ๐—œ๐—ฟ๐—ฒ๐—ป๐—ฒ ๐—ข๐—บ๐—ฏ๐—ฒ๐—ป๐—ถ vifaa vya kisasa vya usafi wa mazingira, ikiwemo toroli, reki, fagio imara, ndoo na vifaa kinga, kwa lengo la kumuwezesha katika huduma yake ya kujitolea kufanya usafi katika mitaa mbalimbali ndani ya Mkoa wa Dar es salaam.

Vifaa hivyo kwa pamoja vina thamani ya shilingi 320,000/= na makabidhiano hayo yamefanyikia katika Ofisi ya Mbunge iliyopo Gezajuu jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, tarehe 15 Oktoba 2026.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Mbunge, Katibu wa Mbunge Ndugu. ๐—”๐—บ๐—ถ๐—ป ๐—”๐—น๐—น๐˜† amesema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Mbunge Sanga katika kuwawezesha vijana kiujumla kwenye masuala ya kiuchumi, michezo na kufungua milango ya fursa.

Mbunge Sanga amefanya hivyo akiamini kuwa Mwanadada Irene ataweza kujiajiri katika shughuli za usafi na hata kuajiri na wenzake kwa siku za mbeleni huku akisisitiza kuwa hatua hiyo ni katika Kuboresha Afya ya Jamii kwakuwa Mazingira safi yanapunguza magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na kuhara.

Aidha, Sanga ametoa wito kwa Vijana wengine kutumia fursa hiyo kama Irene kwakuwa ni sehemu ya kuzalisha na kukuza Uchumi wa Mtaa kupitia huduma ya usafi kwakuwa inaweza kuwa fursa ya biashara endelevu inayolipa na inahitajika kila siku.
 
Tutampa 1B kutoka kwenye bajet ya el nino kama motisha binti anajituma soon tunaweza mpa nafasi uku chaman
 
Back
Top Bottom