Irente, Lushoto: Je, wajua chanzo cha jina Irente?

Irente, Lushoto: Je, wajua chanzo cha jina Irente?

Wajerumani wako makini sana, walijaribu mazao mengi lakini walishangaa sana kuona udongo wa Lushoto umestawisha viazi vya Ireland, apples, pears, strawberries nk.

Nisikiavyo waliacha rupia nyingi Lushoto.
 
wajerumani waliujenga huu mji kwa weredi zaidi ,Pia udongo unaopatikana hapa una rutuba ya kutosha.
 
Wajerumani wako makini sana, walijaribu mazao mengi lakini walishangaa sana kuona udongo wa Lushoto umestawisha viazi vya Ireland, apples, pears, strawberries nk.

Nisikiavyo waliacha rupia nyingi Lushoto.
... Lushoto ndio mjerumani alitaka kujenga HQ yake sema WW1 ikamtimua.
 
Mwaka 1896 Kampuni ya kikoloni ya serikali ya ujerumani ya Germany East Africa Plantation (Deutsche-Ostafrikanische Plantagenge Schellshaft) walianzisha shamba la majaribio ya kilimo cha kahawa kwenye eneo ambalo kwa sasa linajulikana kwa jina la Irente.

Mashamba mengine ambayo yalianzishwa kipindi hicho ni Gare, Maweni, Sakharani na Mazumbai. Kusudi lilikuwa ni kufanya jaribio la zao hili lakini kutokana na ukosefu wa rotuba ya udongo zao la kahawa lilitelekezwa mwaka 1914.

Baada ya Ujerumani kupoteza koloni lake kwa Mwingereza mwaka 1918 shamba hili lilimikiwa na raia kutoka Ugiriki, Bwana W.J Tamé. Na baada ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 shamba hili liliuzwa kwa Kanisa la Kilutheri Tanzania (Tanzania Lutheran Church).

Inasemekana neno Irente Farm lilitokana na kirai (phrase) "I rented a Farm" na hivyo jina Irente likatokana na jina "I rented". Kutokana na mazungumzo ya lugha ya kingereza wakati huo baadhi ya Waswahili walibadilisha "I rented" kuwa ‘Irente’. View attachment 1459919

Jr[emoji769]
Kumbe!
 
Bila WWI tungekuwa taifa mojawapo liliendelea sana. Maana Mjerumani alipafanya Kama nyumbani kwake na tungechelewa kupata uhuru. Na ccm isingekuwepo kabisa maana tungepata uhuru kwa mtutu.

Na tungekuwa vizuri.

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
imefanana na ya Kyela kuna eneo linaitwa Bujonde jina Bujonde” limetokana na neno beyond ambalo Wanyaki wa kyela awakulinyaka vizuri kutoka kwa mzungu...sina uwakika nilipewa kahistori na Mmjomba mda kidogo
 
Ngoja wiki ijayo nikaoshe nyota hapo
...nenda lakini nakushauri sio mahali salama sana kwenda na watoto wa chini ya miaka sita (kwa mtaamo wangu)....pako juu sana na hakuna kingo za maana sana kwa usalama wa watoto wadogo hasa pale unapoelekea kwenye view point, karibu na vyumba vya kulala! Kumbuka soda tunayonunua huku buku mbili kule ni dola 10! otherwise it is a very beautiful place!
 
Gare nilipapenda sana yale mazingira ya kimissionari yalikuwa yanavutia sana

Irente Primary School - Watoto wasioona
Nakumbuka walikuja shuleni kwetu kuimba ( huwa sisahau sauti zao nililia sana siku ile. Niliwaonea huruma sana nikajiuliza kwa nini wengine wako hivi! Waliamba vizuri sana ukisikia talanta ni wale watoto)
Ndipo nilipoanza kuipenda 'Tuimbe Sote-RTD'
Kumbe wewe mkongwe eeh!
 
Back
Top Bottom