Boran Jakutay
Senior Member
- Apr 8, 2023
- 110
- 259
Kijana Carlos Mwamilinga aliyekuwa na miaka 37, amekutwa amejinyonga kwa kamba katika chumba alichokuwa akiishi eneo la Njiapanda ya Mtwivila kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni kutingwa na mawazo kupita kiasi kutokana na kuachana na mkewe mwezi mmoja uliopita.
Marafiki na majirani wa marehemu, wamebainisha kwamba, kijana huyo baada ya kuachana na mkewe, akaanza kunywa pombe kali huku akionekana mwenye mawazo sana.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Idunda, Elisius Mbilinyi, amesema sababu ya moja kwa moja ya kijana huyo kujinyonga haijafahamika, huku akibainisha kwamba marehemu alikuwa akiishi peke yake baada ya kuachaba na mkewe.
Chanzo: Azam TV