Iringa: Marufuku watoto chini ya miaka 9 kupanda bodaboda

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2009
Posts
16,908
Reaction score
19,123
Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoani Iringa, kimepiga marufuku watoto chini ya umri wa miaka tisa kupanda bodaboda.

Mkuu wa Kitengo hicho, ASP Yusuph Kameta amesema ni kosa kisheria kwa mtoto chini ya umri huo kupanda bodaboda.

Hata hivyo, wazazi na walezi wengi ndio wanaoongoza kuwapakia watoto wao kwenye usafiri wakati wa kwenda na kurudi shuleni bila kujali usalama wao.

“Ni marufuku, mtoto mdogo hawezi kuvaa kofia ngumu hata akivaa kabla hajaanguka chini, kofika inakuwa imeshafika. Ni hatari sana,” amesema Kamota na kuongeza;

“Mzazi unaachaje mtoto wako mdogo apande bodaboda? Halafu wengine wanawapakia mpaka watoto wawili au watatu bila kujali kabisa, likitokea lolote unapata misiba miwili.”

Amesema wanaendelea kutoa elimu kwa wazazi juu ya kuwasaidia watoto wao ili badala ya kutumia usafiri huo watumie bajaji, daladala au mabasi ya shule.

Kwa upande wao baadhi ya wazazi wamesema majukumu mengi yamekuwa yakichangia wengi kuona bodaboda kama njia rahisi ya usafiri kwa watoto wao.

“Mama wa watoto wangu yupo bize na mie ni dereva bodaboda ndio maana huwa nawapeleka mwenyewe, sikujua kama ni kosa,” amesema Jones Ngeli, mkazi wa Kihesa.

Mwananchi
 
Du bodaboda vwatakosa ulaji maana mama akiamka apaka bluebad kwenye mkate, mtoto akiwa anakunywa chai yeye anahesabu hela ya bodaboda. Akishamkabidhi mtoto kwa bodaboda anarudi kubandika maharage jikoni.
 
Hata miaka 10 bado ni mtoto sana. Wapandishwe bajaji wajameni. Tuwapende na kuwalinda watoto wetu
Bajaji zipo town tu. Mtu anakaa kilimahewa, nduli, lugalo, mbigiri. Hizo Bajaj anazipata wapi.

Wanaotoa maamuzi utafikiri hawaishi bongo.
 
Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoani Iringa, kimepiga marufuku watoto chini ya umri wa miaka tisa kupanda bodaboda. Mkuu wa Kitengo hicho, ASP Yusuph Kameta amesema ni kosa kisheria kwa mtoto chini ya umri huo kupanda bodaboda.

Hata hivyo, wazazi na walezi wengi ndio wanaoongoza kuwapakia watoto wao kwenye usafiri wakati wa kwenda na kurudi shuleni bila kujali usalama wao.

“Ni marufuku, mtoto mdogo hawezi kuvaa kofia ngumu hata akivaa kabla hajaanguka chini, kofika inakuwa imeshafika. Ni hatari sana,” amesema Kamota na kuongeza;

“Mzazi unaachaje mtoto wako mdogo apande bodaboda? Halafu wengine wanawapakia mpaka watoto wawili au watatu bila kujali kabisa, likitokea lolote unapata misiba miwili.”

Amesema wanaendelea kutoa elimu kwa wazazi juu ya kuwasaidia watoto wao ili badala ya kutumia usafiri huo watumie bajaji, daladala au mabasi ya shule.
 
Juzi juzi nilikuwa namwangalia junia akirudishwa kutoka shule, nikajiuliza hivi hawa watoto hawasinzii njiani kwenye hizi bodaboda.

Anyways, uamuzi siyo mbaya japo utakuwa na changamoto zake
 
Bila kusahau madogo wa panya road ipogolo mnavyobebaga mishkaki vitoto vya watu kutokea kule maliasili mkome tafadhali
 
Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoani Iringa, kimepiga marufuku watoto chini ya umri wa miaka tisa kupanda bodaboda.

Mkuu wa Kitengo hicho, ASP Yusuph Kameta amesema ni kosa kisheria kwa mtoto chini ya umri huo kupanda bodaboda.

Hata hivyo, wazazi na walezi wengi ndio wanaoongoza kuwapakia watoto wao kwenye usafiri wakati wa kwenda na kurudi shuleni bila kujali usalama wao.

“Ni marufuku, mtoto mdogo hawezi kuvaa kofia ngumu hata akivaa kabla hajaanguka chini, kofika inakuwa imeshafika. Ni hatari sana,” amesema Kamota na kuongeza;

“Mzazi unaachaje mtoto wako mdogo apande bodaboda? Halafu wengine wanawapakia mpaka watoto wawili au watatu bila kujali kabisa, likitokea lolote unapata misiba miwili.”

Amesema wanaendelea kutoa elimu kwa wazazi juu ya kuwasaidia watoto wao ili badala ya kutumia usafiri huo watumie bajaji, daladala au mabasi ya shule.

Kwa upande wao baadhi ya wazazi wamesema majukumu mengi yamekuwa yakichangia wengi kuona bodaboda kama njia rahisi ya usafiri kwa watoto wao.

“Mama wa watoto wangu yupo bize na mie ni dereva bodaboda ndio maana huwa nawapeleka mwenyewe, sikujua kama ni kosa,” amesema Jones Ngeli, mkazi wa Kihesa.

Mwananchi
Mimi kila siku naamini kuwa ajali za barabarani huku kwetu kwa asilimia 65 ni uzembe wa wasimamizi wa vyombo, wasimamizi wa sheria na kanuni pamoja na wasimamizi/mamlaka za miundombinu.
TanPol kitengo cha Usalama Barabarani ndio wamelala sana sana.
Hawa wakitimiza majukumu yao kiuadilifu kwa asilimia 50 tuu,tutapunguza ajali kwa kiwango kikubwa sana.
 
Ni vyema ila sidhani Kama ni rahisi kiutendaji.
 
Mimi kila siku naamini kuwa ajali za barabarani huku kwetu kwa asilimia 65 ni uzembe wa wasimamizi wa vyombo, wasimamizi wa sheria na kanuni pamoja na wasimamizi/mamlaka za miundombinu.
TanPol kitengo cha Usalama Barabarani ndio wamelala sana sana.
Hawa wakitimiza majukumu yao kiuadilifu kwa asilimia 50 tuu,tutapunguza ajali kwa kiwango kikubwa sana.
unaposema uzembe wa wasimamizi ina maana unataka tuongozwe siku zote? kwa nini tusijiongoze wenyewe? au elimu bado haitoshi?.
 
Sheria zipo,zinasimamiwa vilivyo???
Rushwa imetawala ndio maana watu hatuogopi kuvunja sheria za usalama barabarani.
Wasimamizi wetu wameshindwa kusimamia sheria,kanuni,miongozo na taratibu,ndio maana tumekuwa taifa la mkwamo.
 
Bajaji zipo town tu. Mtu anakaa kilimahewa, nduli, lugalo, mbigiri. Hizo Bajaj anazipata wapi.

Wanaotoa maamuzi utafikiri hawaishi bongo.
Waanashangaza sanaa yaan. Khaaaah
 
Bila kusahau madogo wa panya road ipogolo mnavyobebaga mishkaki vitoto vya watu kutokea kule maliasili mkome tafadhali
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Juzi juzi nilikuwa namwangalia junia akirudishwa kutoka shule, nikajiuliza hivi hawa watoto hawasinzii njiani kwenye hizi bodaboda.

Anyways, uamuzi siyo mbaya japo utakuwa na changamoto zake
Wanalala kabisa!
 
Back
Top Bottom