Uchaguzi 2020 Iringa: Mgombea Urais wa chama cha ADC, Queen Sendiga adai kupigwa makofi na watu wasiojulikana na kuvunjiwa kioo cha gari lake

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
MGOMBEA urais wa chama cha ADC, Queen Sendiga adai kupigwa makofi na watu wasiojulikana na kuvunjiwa kioo cha gari lake akiwa katika maeneo ya stendi kuu ya zamani ya Manispaa ya Iringa kuendelea na mikutano yake ya hadhara ya kampeni .

Akizungumza mara baada ya tukio hilo leo mgombea huyo alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 10 jioni wakati akielekea katika viwanja vya Stendi kuu ya zamani ya mabasi yaendayo mikoani eneo ambalo pia chama cha mapinduzi (CCM) walikuwa na mkutano wa kampeni za mgombea wa udiwani kata ya Kitanzini Miyomboni .

Alisema kuwa jana kwa mujibu wa ratiba alikuwa ana mikutano yake ya kampeni katika mkoa wa Iringa katika halmashauri ya Manispaa ya Iringa na asubuhi baada ya kuwasili Iringa alikutana na matangazo ya mgombea udiwani na ndipo alipotoa taarifa tume ya taifa ya uchaguzi kulalamikia suala hilo

" Mimi kabla ya kuwasilisha malalamiko mkurugenzi wa tume ya Taifa ya uchaguzi Bwana Mahela kuelezea vurugu ambazo nimekutana nazo jimbo la Iringa mjini niliendelea na ratiba zangu za kampeni za kuzunguka mitaano kama sokono na maeneo mengine kuomba kura japo tayari mgombea wangu wa nafasi ya ubunge jimbo la Iringa mjini Daud Masasi ambae pia ni kamishina wa ADC mkoa wa Iringa aliwasilisha malalamiko hayo kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini" alisema

Kuwa ameshangazwa na kusikitishwa na tukio la vijana kuvamia gari lake la matangazo na kuvunja kioo cha mbele cha gari hilo na wengine kumzingira na kumpiga makofi yeye wakati akihoji sababu ya gari lake kuvunjwa kioo wakati akielekea eneo hilo katika mkutano.

Hata hivyo alisema kuwa katika vurugu hizo gari la matangazo na vijana waliokuwepo katika gari hilo ndio ambao wameshambuliwa sana na yeye wameishia kumsukuma na kumzaba makofi wakati wa mvutano huo .

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Juma Bwire alipotafutwa na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu alisema hajapata taarifa hizo zaidi ya kusikia kutoka kwa mwandishi hivyo anafuatilia
 
Kumbe hadi huyu mama anaogopwa na wale nzi wa kijanii?
 
Swali: Mpaka kupigwa makofi, je hakuwa na walinzi? Mtu apenye ampige makofi asikamatwe na walinzi? Muangalie sana huyu binti anatafuta "kiki" kwa niaba ya CCM
 
Huyo mgombea n pisi Kali,napenda anavyosuka simple (twende kilioni)
 
Wagombea walipaswa wawe na walinzi wa serikali, sasa imekuwaje tena?
 
Aliyekuambia wasiojulikana wanapiga makofi na kukuacha hv hv ni nani ???

acha masihara ww
 
Hutu tu vyama ni kichefu chefu tu hawa ndo hutumika kuangamiza wapinzani kamati ya maadili!! Hovyo sana hawa
Pamoja na mapungufu yao wanahaki ya kuheshimiwa na kulindiwa utu wao pia.

Kama tunahubiri haki ni vyema tukaihubiri haki kwa misingi yake yote.

Kupigwa makofi kwa mgombea siyo jambo la kistaarabu hata kidogo.

Na siasa za namna hii wanazo ccm

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 

Watajijua wenyewe na maccm yenzao huko hawa ndo wapiga kura ya maamuzi huko kamati ya maadili hovyo sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…