Uchaguzi 2020 Iringa: Mgombea Urais wa chama cha ADC, Queen Sendiga adai kupigwa makofi na watu wasiojulikana na kuvunjiwa kioo cha gari lake

Watajijua wenyewe na maccm yenzao huko hawa ndo wapiga kura ya maamuzi huko kamati ya maadili hovyo sana
Mkuu ilani yetu inazungumzia kutenda haki kwa watu wote.

Kuvunjwa kwa haki za John ni precedent ya kuvunjwa kwa haki za Swaibu pia.

Kukaa kwetu kimya ni kuunga mkono na wenzetu wakae kimya tutakapovunjiwa haki zetu sisi pia

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Chadema ndio wenye tabia za kupiga watu makofi, muache.
 
Afadhali ya Kofi kuliko
ndugu huo ndio ukweli ukisikia mtu kakutana na wasiojulikana ujue huyo ni marehemu tayari !

aliyemuambia wanapiga makofi tu ni nani ?
aache masihara kabisa
😀😀😄😄😁😆🤣😇
Au labda hata ngumi tu
 
Yule bodigadi wake mwanamama aliyepanda hewani alishindwa kuzuia Kofi?
 
Attachments

  • images (8).jpeg
    images (8).jpeg
    11.7 KB · Views: 2
  • images (7).jpeg
    images (7).jpeg
    22.2 KB · Views: 2
  • images (6).jpeg
    images (6).jpeg
    22.2 KB · Views: 2
MGOMBEA urais wa chama cha ADC, Queen Sendiga adai kupigwa makofi na watu wasiojulikana na kuvunjiwa kioo cha gari lake akiwa katika maeneo ya stendi kuu ya zamani ya Manispaa ya Iringa kuendelea na mikutano yake ya hadhara ya kampeni .

Akizungumza mara baada ya tukio hilo leo mgombea huyo alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 10 jioni wakati akielekea katika viwanja vya Stendi kuu ya zamani ya mabasi yaendayo mikoani eneo ambalo pia chama cha mapinduzi (CCM) walikuwa na mkutano wa kampeni za mgombea wa udiwani kata ya Kitanzini Miyomboni .

Alisema kuwa jana kwa mujibu wa ratiba alikuwa ana mikutano yake ya kampeni katika mkoa wa Iringa katika halmashauri ya Manispaa ya Iringa na asubuhi baada ya kuwasili Iringa alikutana na matangazo ya mgombea udiwani na ndipo alipotoa taarifa tume ya taifa ya uchaguzi kulalamikia suala hilo

" Mimi kabla ya kuwasilisha malalamiko mkurugenzi wa tume ya Taifa ya uchaguzi Bwana Mahela kuelezea vurugu ambazo nimekutana nazo jimbo la Iringa mjini niliendelea na ratiba zangu za kampeni za kuzunguka mitaano kama sokono na maeneo mengine kuomba kura japo tayari mgombea wangu wa nafasi ya ubunge jimbo la Iringa mjini Daud Masasi ambae pia ni kamishina wa ADC mkoa wa Iringa aliwasilisha malalamiko hayo kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini" alisema

Kuwa ameshangazwa na kusikitishwa na tukio la vijana kuvamia gari lake la matangazo na kuvunja kioo cha mbele cha gari hilo na wengine kumzingira na kumpiga makofi yeye wakati akihoji sababu ya gari lake kuvunjwa kioo wakati akielekea eneo hilo katika mkutano.

Hata hivyo alisema kuwa katika vurugu hizo gari la matangazo na vijana waliokuwepo katika gari hilo ndio ambao wameshambuliwa sana na yeye wameishia kumsukuma na kumzaba makofi wakati wa mvutano huo .

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Juma Bwire alipotafutwa na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu alisema hajapata taarifa hizo zaidi ya kusikia kutoka kwa mwandishi hivyo anafuatilia
Pole sana ndugu mgombea,

Hapo ndipo vijana wa ccm walipofikia
Mnaposhauriwa kuungana kusimamisha mgombea mmoja ninyi kama wapinzani tunamaanisha

Maana ccm huwa wanawashabikia na kuwatumia ili upinzani usipate nguvu kwa manufaa yao.

Na wakishamaliza kazi yao basi wanawatia makofi kama hivi

Saizi yao kwa sasa ni Chadema,
waungeni chadema mkono na maumivu yenu yapoe

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
MGOMBEA urais wa chama cha ADC, Queen Sendiga adai kupigwa makofi na watu wasiojulikana na kuvunjiwa kioo cha gari lake akiwa katika maeneo ya stendi kuu ya zamani ya Manispaa ya Iringa kuendelea na mikutano yake ya hadhara ya kampeni .

Akizungumza mara baada ya tukio hilo leo mgombea huyo alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 10 jioni wakati akielekea katika viwanja vya Stendi kuu ya zamani ya mabasi yaendayo mikoani eneo ambalo pia chama cha mapinduzi (CCM) walikuwa na mkutano wa kampeni za mgombea wa udiwani kata ya Kitanzini Miyomboni .

Alisema kuwa jana kwa mujibu wa ratiba alikuwa ana mikutano yake ya kampeni katika mkoa wa Iringa katika halmashauri ya Manispaa ya Iringa na asubuhi baada ya kuwasili Iringa alikutana na matangazo ya mgombea udiwani na ndipo alipotoa taarifa tume ya taifa ya uchaguzi kulalamikia suala hilo

" Mimi kabla ya kuwasilisha malalamiko mkurugenzi wa tume ya Taifa ya uchaguzi Bwana Mahela kuelezea vurugu ambazo nimekutana nazo jimbo la Iringa mjini niliendelea na ratiba zangu za kampeni za kuzunguka mitaano kama sokono na maeneo mengine kuomba kura japo tayari mgombea wangu wa nafasi ya ubunge jimbo la Iringa mjini Daud Masasi ambae pia ni kamishina wa ADC mkoa wa Iringa aliwasilisha malalamiko hayo kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini" alisema

Kuwa ameshangazwa na kusikitishwa na tukio la vijana kuvamia gari lake la matangazo na kuvunja kioo cha mbele cha gari hilo na wengine kumzingira na kumpiga makofi yeye wakati akihoji sababu ya gari lake kuvunjwa kioo wakati akielekea eneo hilo katika mkutano.

Hata hivyo alisema kuwa katika vurugu hizo gari la matangazo na vijana waliokuwepo katika gari hilo ndio ambao wameshambuliwa sana na yeye wameishia kumsukuma na kumzaba makofi wakati wa mvutano huo .

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Juma Bwire alipotafutwa na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu alisema hajapata taarifa hizo zaidi ya kusikia kutoka kwa mwandishi hivyo anafuatilia
Yaani mgomgea kachapwa makofi? #ONLY IN TANZANIA na vyombo vya dola vipo tu vinaangalia
 
Hawa wagombea si wanapewa ulinzi na serikali? Mlinzi wake alikua wapi?
 
mzee wa ubwabwa yupo wapi simsikii kabisa pumzi imekata nini....naona anashindwa na mama sandiga. Mama sandiga anaonekana kuwa na pumzi ya katafuta kura....safi sana ni mfano mzuri kwa kina mama
 
Back
Top Bottom