KERO Iringa Mjini tunapandishiwa nauli za daladala njia kutoka Stendi ya Zamani - Igumbilo - Stendi Kuu

KERO Iringa Mjini tunapandishiwa nauli za daladala njia kutoka Stendi ya Zamani - Igumbilo - Stendi Kuu

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
photo_2026-08-17_14-09-36.jpg
Wakazi wa Iringa Mjini tunapandishiwa nauli za daladala katika njia kutoka Stendi ya Zamani kupitia Igumbilo hadi Stendi Kuu ya Mabasi na Viwengi, magari yanayofanya safari katika njia hii yamekuwa yakitoza nauli kubwa kuliko viwango vilivyowekwa na LATRA.

Kwa mujibu wa nauli nilizopewa, tofauti ni kama ifuatavyo:
  • Stendi ya Zamani – Kwendiuka (km 7): LATRA Sh700, lakini abiria tunatozwa Sh1,000.
  • Stendi ya Zamani – Lusingo (km 11): LATRA Sh800, lakini tunatozwa Sh1,000.
  • Stendi ya Zamani – Igumbilo Mtaani (km 12.5): LATRA Sh800, lakini tunatozwa Sh1,000.
  • Stendi ya Zamani – Igumbilo Stendi Kuu (km 14): LATRA Sh800, lakini tunatozwa Sh1,000.

Naomba LATRA na mamlaka husika zifuatilie suala hili na kuhakikisha viwango vya nauli vilivyowekwa vinazingatiwa, kwa sababu abiria tunaendelea kubeba mzigo wa malipo ya ziada kila siku.
 
Awamu hii hakuna wa kuwatetea aisee,kitu kama hakimpandishi mtu kisiasa hana time na nyie endeleeni kufa na tie shingoni.
 
pole sana mnyarukolo ila tukiachana na yote kwa yote kwa kweli sisi zetu ni dua tu
 
Back
Top Bottom