Iringa: Mkazi wa Dar akamatwa baada ya kuzidiwa akisafirisha Dawa za Kulevya alizomeza

View attachment 2576220
Baadhi ya pipi za heroine zilizotolewa kwa njia ya haja kubwa na mtuhumiwa Mwasema Rashid baada ya kuwaambia ukweli Madaktari kuwa alikuwa akisafirisha dawa hizo kwa kuzimeza.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa linamshikilia Mwasema Rashid (37) Mkazi wa Tabata Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin alipokuwa akisafirisha kutoka nchini Msumbiji.

Akizungumza na Mwananchi jana Aprili 3, 2023 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa machi 31, 2023 majira ya saa tano usiku Kijiji cha Mtandika Wilaya ya Kilolo akidaiwa kuelekea jijini Dar es Salaam alikokuwa akipeleka dawa hizo.

Kulingana na Bukumbi, mtuhumiwa alisafiri kutoka Dar es Salaam Machi 17, 2023 kwa kutumia usafiri wa ndege kuelekea Msumbiji, Machi 30, 2023 alirejea kupitia Jiji la Mbeya kwa kutumia usafiri wa gari

Bukumbi amesema mtuhumiwa alijulikana kuwa na dawa hizo za kulevya alipoenda Hospitali ya Mtandika kutibiwa baada ya kuhisi maumivu ya tumbo akiwa njiani na hali yake ilivyozidi kuwa mbaya Aprili 2, 2023 aliamua kuongea ukweli kwa madaktari kuwa alimeza pipi za dawa za kulevya aina ya heroin na hatimaye kutoa dawa hizo kwa njia ya haja kubwa.

"Hadi sasa mtuhumiwa ameshatoa pipi 58 za heroin kupitia njia ya haja kubwa chini ya uangalizi wa Madaktari na Askari Polisi, tunakamilisha upelelezi na baada ya hapo mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani", amesema Bukumbi.

Chanzo: Mwananchi
Mwamba nae kajizungusha sana, kupita Mbeya kutokea msumbuji ni njia ndefu mno, alikuwa apite Mtwara tu
 
Punda Wamerudi Kwa Kazi, Muhari Unaimaliza Tanzania
Mzilankende Hakutaka Kubembeleza
 
Mwamba nae kajizungusha sana, kupita Mbeya kutokea msumbuji ni njia ndefu mno, alikuwa apite Mtwara tu
Kama ametoka nazo Beira au Maputo njia rahisi na ya haraka kufika Dar (masaa 72) ni Malawi. Kuna kipindi jimbo la kaskazini linakuwa halina mawasiliano na Beira aidha kwa mvua au waasi.
 
View attachment 2576220
Baadhi ya pipi za heroine zilizotolewa kwa njia ya haja kubwa na mtuhumiwa Mwasema Rashid baada ya kuwaambia ukweli Madaktari kuwa alikuwa akisafirisha dawa hizo kwa kuzimeza.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa linamshikilia Mwasema Rashid (37) Mkazi wa Tabata Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin alipokuwa akisafirisha kutoka nchini Msumbiji.

Akizungumza na Mwananchi jana Aprili 3, 2023 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa machi 31, 2023 majira ya saa tano usiku Kijiji cha Mtandika Wilaya ya Kilolo akidaiwa kuelekea jijini Dar es Salaam alikokuwa akipeleka dawa hizo.

Kulingana na Bukumbi, mtuhumiwa alisafiri kutoka Dar es Salaam Machi 17, 2023 kwa kutumia usafiri wa ndege kuelekea Msumbiji, Machi 30, 2023 alirejea kupitia Jiji la Mbeya kwa kutumia usafiri wa gari

Bukumbi amesema mtuhumiwa alijulikana kuwa na dawa hizo za kulevya alipoenda Hospitali ya Mtandika kutibiwa baada ya kuhisi maumivu ya tumbo akiwa njiani na hali yake ilivyozidi kuwa mbaya Aprili 2, 2023 aliamua kuongea ukweli kwa madaktari kuwa alimeza pipi za dawa za kulevya aina ya heroin na hatimaye kutoa dawa hizo kwa njia ya haja kubwa.

"Hadi sasa mtuhumiwa ameshatoa pipi 58 za heroin kupitia njia ya haja kubwa chini ya uangalizi wa Madaktari na Askari Polisi, tunakamilisha upelelezi na baada ya hapo mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani", amesema Bukumbi.

Chanzo: Mwananchi

Ushahidi huo utunzwe sasa.maana sometimes hizo pipi zikifikishwa kwa mkemia mkuu zinageukaga kuwa pipi kifua halisi
 
Unadhani mkemia mkuu hajipendi kwa kuzuia mzigo wa wakuu.....hiyo imeisha mzigo umefika salama licha ya kupitia changamoto ndogo ndogo
 
Alifika tayari Mbeya, kulikuwa na haja gani ya kuendelea kuutunza mzigo tumboni?
 
Sina uzoefu na hizi mambo ila nimesafiri sana ila sijawahi kukaguliwa kwa experience hiyo kama hazina harufu ya kuzitambulisha hata kwenye beg dogo angebeba kisha anaweka kwenye carriar ya gari ya ndani na hakuna baya tena yaani unasafirisha utajiri kitajiri na ukipewa mpunga unapita kidimbwi au samakisamaki unakula raha hamna shida
 
Siku utakayobeba ndio utakayokaguliwa
 
Jiografia imenichanganya kidogo, Msumbiji inapakana na mikoa ipi?

Ama mimi ndo sielewi hapa.

Hii kitu ni uwongo mtupu walahi, maana alisha vuka boda na kwa nini hakutafuta gesti akazitoa?
Alafu Msumbiji haiko huko kama avyo dai mleta mada!
Newzzz za kahawa![emoji1787][emoji1787]
 
Hayo madawa atarudishiwa na Safari itaendelea, kuanzia uzaliwe umewahi kumsikia muuza nganda amehukumiwa kufungwa Tanzania? Hata wale wakionyang'anywa Mali zao na mwamba kwenye plea bargain wanarudishiwa
 
Back
Top Bottom