Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Muda wa kuswali wapunguzwa Mkoani Iringa, kuanzia jana, muda wa kuswali katika nyumba za ibada umepunguzwa kutoka zaidi ya dakika 30 za awali hadi kati ya dakika 10 na 15 siku ya Ijumaa.
Shehe wa Mkoa wa Iringa, Abri Said alisema utekelezaji wa maelekezo hayo ulianza jana katika misikiti yote mkoani humo ikiwa ni hatua inayolenga kuunga mkono juhudi za serikali za kukabiliana na wimbi la tatu la covid-19.
“Kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania niwaombe waumini wetu wote mkoani Iringa kuchukua tahadhari kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu ili kuepukana na janga hili hatari,” alisema.
Pamoja na kupunguza muda huo wa ibada, Sheikh Abri alisema waumini watakaoenda misikitini, madrasa na watakaoshiriki shughuli nyingine za dini hiyo, watatakiwa kukaa mbalimbali ikiwa ni hatua nyingine ya kukabiliana na ugonjwa huo.
Kuhusu masuala ya misiba na ndoa, aliwaomba waumini wavumilie kwa kukubali ushiriki wa watu wachache kwa maana ya majirani na familia. “Tukijikinga na kujilinda, tukamtanguliza Mwenyezi Mungu, suala hili litakuwa la muda.
Mwenyezi Mungu atatulinda na tutavuka salama. Tuahirishe mikusanyiko na makongamano yasyo ya lazima,” alisema.