Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu Rucu mkoani Iringa, Rachel Mkubwa amefariki dunia kwa kile kilichodaiwa kubakwa hadi kufa na watu wasiojulikana.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Desemba 12 katika Mtaa wa Mhimba B, Kata ya Makorongoni Manispaa ya Iringa.
Akizungumza na Mwananchi Digital, Diwani wa Kata hiyo, Thadeus John amethibitisha kutokea kwa kifo hicho huku akisema mpaka sasa wanasubiri taarifa rasmi za Jeshi la Polisi kuhusiana na tukio hilo.
Diwani huyo amesema wiki iliyopita katika eneo hilo mwili wa kijana mmoja nao uliokotwa mtaroni akiwa amefariki dunia, huku amefungwa kamba.
βHali hii imeanza kuibua hofu kwa wakazi wa mtaa huu na kifo cha huyu mwanafunzi, tunaishi na wanafunzi wengi mtaani sasa mambo kama haya yakianza kuibuka, yanazua hofu kubwa,β amesema diwani John.