BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Mafundi wakijenga Kizimba ndani ya Bwawa la Nzivi, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa kwa ajili ya ufugaji samaki
Uwekezaji mkubwa wa ufugaji samaki kwa njia ya vizimba imetajwa kuwa ni fursa kubwa ya uwekezaji katika Bwawa la Nzivi wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Hatua ya uwekezaji huo mkubwa umekuja huku Serikali ya Mkoa wa Iringa chini ya Mkuu wa Mkoa Queen Sendiga imeendelea kuhamasisha wananchi wa mkoa huo kuwekeza Katika mabwawa ya samaki na Kilimo cha Parachichi.
Akizungumzia juu ya uwekezaji huo unaendelea Bwawa la Nzivi Mufindi, Mjasiriamali Maria Makombe amesema kuwa ufugaji wa kizimba ama vizimba umekuwa ukifanyika katika ziwa ama mabwawa na umekuwa na manufaa makubwa sana.
Amezitaja faida kubwa katika ufugaki wa vizimba kuwa ni kukuza biashara ya samaki kwa kiasi kikubwa, kutengeneza ajira kwa wauzaji wa samaki maana kwa kutumia vizimba pindi unapoanza kuvuna unavuna samaki wengi kwa wakati mmoja.
Pia kukuza uchumi wa eneo husika maana vizimba vinavutia watu wengi kuwekeza hivyo sehemu husika lazima itafaidika na ajira na mapato pia.
Mjasiriamali Maria Makombe
Aidha, ufugaji huo ni sehemu ya utalii kwa Wilaya ya Mufindi na Mkoa wa Iringa maana hakuna sehemu ndani ya Iringa ufugaji huo unafanyika wakati kuna mabwawa mengi zaidi.
Maria amesema kuwa wanawake wanapaswa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya shughuli za ujasiriamali kama hizo kupitia rasirimali zinazowazunguka kwa Ardhi, mito na nyingine nyingi.
Kuwa iwapo wanawake wataunga mkono jitihada hizo za Rais kwa kufanya kazi ni wazi maendeleo yataonekana na kweli azma ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kazi iendelee itafanikiwa Kwa kila mmoja wetu.
Source: Matukio Daima