Iringa: Wapiga Debe Waanza Kuondolewa Rasmi Kwenye Stand -Hongera Serikali

Iringa: Wapiga Debe Waanza Kuondolewa Rasmi Kwenye Stand -Hongera Serikali

Faana

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
38,657
Reaction score
44,759
Jana 2.9.22 majira ya saa saba mchana police walionekana kuwakamata wapiga debe maeneo mbalimbali ya mji wa Iringa ikiwemo pale daraja la mto Ruaha, polisi hao walimkimbiza mmoja wa wapiga debe naye akakimbila kwa kasi kuelekeo unakotokea mto Ruaha.

Hata hivyo polisi hao hawakukata tamaa wakaenda naye hata walipofika mbele kukawa na watu wengine wanaoga ndani ya mto Ruaha walipoona mtu anapita anakimbia na nyuma yake wanakuja polisi, na wao wakatoka kwenye maji wakaungana naye mbio kuelekea upande allikokuwa anakwenda huyo aliyeanza kukimbizwa na polisi huku wameacha nguo kando ya mto bila kujua aliyeko mbele anakimbizwa kwa kosa gani huku polisi wakizidi kuongezeka.

Huu ni mwanzo mzuri wa kupunguza kero kwenye stand zza mabasi.
 
Kwamba mwenye nguo anamkimbiza asiye vaa chochote [emoji23][emoji23]. Weka video kwanza nitarudi kihitimisha
 
Tupe video kwanza. Patamu hapo. Kile kimto kina mamba na viboko kile.
 
Wapiga debe asilimia kubwa ni wezi, wahuni, matapeli, walaghai na walanguzi. Acha waondolewe ili watafute kazi nyingine na stand zetu ziwe salama.
 
Watarudi tu hao

Nguvu ya soda tu hiyo

Ova
 
Back
Top Bottom