Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeendesha mafunzo ya siku mbili kwa watendaji kwa ngazi ya halmashauri na majimbo katika halmashauri ya Iringa huku watendaji hao wakisistizwa kwenda kuifanyia kazi elimu watakayoyapata kwenye ngazi za chini.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Afisa muandikishaji Jimbo la Ismani na kalenga ambaye ndie alikuwa mgeni rasmi Bi. Beatrice Kabambagushi amesema watendaji wanatakiwa kuzingatia elimu hiyo kwani mafunzo hayo yanahusu namna bora ya ujazaji wa fomu, kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura pamoja na matumizi sahihi ya vifaa vya uandikishaji kwa wapiga kura.
Kwa mafunzo mtakayopata natarajia mtafanya kazi kwa weredi, juhudi na moyo wa kujituma Ili kufanikisha zoezi hili la kitaifa, "Alisema Beatrice"
Beatrice amewasihi watendaji kuwa na ushirikiano na tume ya Taifa ya Uchaguzi INEC wakati wote wa zoezi huku akisisitiza nidhamu, maadili na uwajibikaji katika kipindi hiki.
Aidha George Mushi ambae ni ARO Jimbo kutoka kalenga amesema kundi Hilo limechaguliwa na tume ya Taifa ya Uchaguzi kusimamia uboreshaji wa daftari la wapiga kura hivyo wameaminiwa
Amesema kalenga na Ismani ina jumla ya ma ARO Jimbo na ma ARO kata 28 hivyo wamejipanga vema.
Kwa upande wake mmoja wa washiriki Bi. Noela Manyai ambae ni ARO kata kutoka kata ya ulanda amesema mafunzo hayo yana umuhimu sana kwao kwani wao wanatakiwa kwenda kuwaekekeza waandikishaji wasaidizi na wasimamizi wa vifaa BVR katika zoezi Hilo la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Mafunzo hayo yalienda sambamba na kuapishwa kwa kula viapo vya utii kwa ajili ya kazi hiyo kwa watendaji hao